Kuhusu Mwandishi
About The Author
Sheikh Fareed Saalih (Haafizh Saalih) Allah amrehemu, alizaliwa katika kijiji kimoja cha Palestina. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi aliacha shule na kufanya kazi Palestina kabla ya kuhamia Kuwait mwanzoni mwa miaka ya 1950. Alipata elimu yake ya sekondari mwishoni mwa miaka ya 1960 huko Jordan, na katikati ya miaka ya 1980 alipata shahada ya Baccalaureus na Shahada ya Uzamili (Masters) katika Masomo ya Kiislamu nchini Pakistan.
Sheikh Fareed Saalih (Haafizh Saalih) May Allah’s mercy be upon him, was born in a Palestinian village. After completing his primary education he left school and worked in Palestine before moving to Kuwait in the early 1950’s. He obtained his secondary education at the end of the 1960’s in Jordan and attained a Baccalaureus degree and Masters in Islamic Studies in Pakistan in the mid 1980’s.
Alikuwa ameoa na alikuwa na watoto kumi na wawili na wajukuu thelathini na wanne.
He was married and had twelve children and thirty-four grandchildren.
Alianza kubeba Da'wah ya Kiislamu kuanzia miaka ya 1950 na aliipa kazi hii kipaumbele kuliko vipaumbele vyote vingine. Alieneza Da'wah nchini Iraq, Jordan, Lebanon, Misri, Pakistan na Tunisia. Alifungwa jela nchini Jordan mwaka 1969 na akahukumiwa kifungo cha maisha. Alifungwa nchini Iraq wakati wa utawala wa Abd Al-Ilah, wakati wa utawala wa Abdul Karim Qasim, Ahmad Hasaan Al-Bakr na Saddam. Pia alifungwa nchini Misri wakati wa utawala wa Sadat, na aliwindwa na mashirika ya kijasusi ya Habib Bourguiba (Tunisia) na Hafez Al-Asad (Syria).