Misikiti, Ya Zamani Na Ya Sasa
The Mosques, Past And Present
Ulinganisho mfupi kati ya hali ya misikiti yetu siku hizi na ile ya Salaf wema unaonyesha kwamba zamani walikuwa wakijikita katika kiini na si mwonekano wa nje, ilhali siku hizi sisi huelekea kujikita katika mwonekano wa nje na kupuuza nafasi muhimu ya msikiti.
A brief comparison between the state of our mosques nowadays and that of the righteous ancestors reveals that in the past they used to concentrate on the essence and not the appearance, whereas nowadays we tend to concentrate on the appearances and disregard the essential role of the mosque.
Kila kitu kinaonekana kuwa kinyume chake: nafasi ya msikiti ilidhibitiwa na kuwa mahali pa kuswali sala tano za faradhi tu, kisha milango yake ikafungwa. Matokeo yake, msikiti umetengwa na maisha, chini ya bendera ya kutenganisha dini na maisha ya kidunia. Serikali, wahubiri na washauri walichukua usukani na kuanza kutenda kwa kufuata miongozo iliyotolewa na watawala ili kurudia kauli mbiu yao ya ‘hakuna siasa katika dini’, wakidai kuwa wao ni maulamaa ambao hawana chochote cha kufanya na siasa, ilhali Uislamu ni dini, na mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimahakama ni sehemu isiyotenganishwa na Uislamu.
Everything seems to be the opposite, the role of the mosque became restricted to the establishing of the five prescribed prayers, and then it would shut its doors. Consequently, the mosque has become isolated from life, under the banner of separating the deen from temporal life. Governments preachers and councillors took centre stage and began acting according to guidelines issued by the rulers to reiterate their slogan of ‘no politics in religion’, claiming that they are the clergymen who have nothing to do with politics, even though Islam is a deen and the political, economic, social and judicial systems are an integral part of Islam.