HITIMISHO
CONCLUSION
Tuliona kwamba manabii, mmoja baada ya mwingine, walitabiri na kubashiri kuhusu nabii wa mwisho: "Torati na manabii hata wakati wa Yohana walihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu".
We saw that the prophets one after another prophesized and foretold about the final prophet "The Law and the prophets until the time of John gave glad tidings of the kingdom of God".
Walitimiza ahadi yao ambayo Mwenyezi Mungu aliwachukulia, nayo ni kuamini na kumsaidia Nabii wa mwisho atakapokuja. {Na (kumbukeni) pale Allaah alipochukua ahadi ya Manabii, akisema: "Hakika nitakapokupeni Kitabu na Hikmah (ufahamu wa Sheria za Allaah, n.k.), kisha atakujieni Mtume (Muhammad) akisadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, lazima mumuamini na mumnusuru." Allaah akasema: "Je, mmekubali na mtachukua juu yenu Ahadi Yangu (ninayofunga nanyi)?" Wakasema: "Tumekubali." Akasema: "Basi shuhudieni; nami niko pamoja nanyi miongoni mwa mashahidi (juu ya hilo)."} (Al-Imraan: 81).
They fulfilled their covenant that God took on them, and that is to believe and support the final prophet when he comes. {And (remember) when Allâh took the Covenant of the Prophets, saying: "Take whatever I gave you from the Book and Hikmah (understanding of the Laws of Allâh, etc.), and afterwards there will come to you a Messenger (Muhammad) confirming what is with you; you must, then, believe in him and help him." Allâh said: "Do you agree (to it) and will you take up My Covenant (which I conclude with you)?" They said: "We agree." He said: "Then bear witness; and I am with you among the witnesses (for this)."} (Al- Emran: 81).
Manabii waliwaeleza watu wao habari za nabii huyu: "Manabii wote na Sheria hadi Yohana walitabiri, na kama mkitaka kukubali, huyu ndiye Eliya aliyetangazwa kuja."
The prophets reported to their people the news of this prophet "all the prophets and the statute until John prophesized, and if you wanted to accept to there is Elijah the proclaimed to come".
Biblia Takatifu (licha ya mabadiliko yanayoipata) imetuhifadhia baadhi ya unabii huu kuhusu nabii huyu mkuu, kwamba ndiye nabii atakayetimiza ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na mkewe Hajiri kwa baraka katika mwanawe Ishmaeli, na ndiye yule "ambaye mataifa watamtii".
The Holy Bible (in spite of the alteration it is exposed to) preserved for us some of these prophecies about this great prophet, that he is the prophet who will fulfill God’s promise to Abraham and his wife Hagar with the blessing in her son Ishmael, and he is the one "that nations submit to".
Yeye ni nabii aliyekuwa kama Musa (PBUH), ambaye Musa aliwaambia watu wake, wana wa Israeli. Ni nabii ambaye utume wake utang'aa karibu na milima ya Paran, na atatoka katika taifa litakalotekeleza Sheria ya ufalme wa Mungu, ambao utaondolewa kutoka kwa wana wa Israeli. "Nao utapewa taifa litakalozaa matunda yake", na hiyo ni kwa sababu "wamenibadilisha na mungu mwingine, na wameniudhi kwa ibada zao za uongo, nami nitawabadilisha kwa taifa jingine, na kwa taifa lisilojua kusoma wala kuandika ambalo liliwaudhi".
He is the prophet who was like Moses (PBUH), whom Moses had told his people, the children of Israel. He is the prophet whose prophet-hood will glitter near the mountains of Paran, and he will be from a nation that will practice the Law of the kingdom of God, which will be taken away from the children of Israel. "And it will be given to a nation that will work for its fruits", and that's because they "replaced me with another God, and they angered me with their fake worships, and I will also replace them with another nation, and with an illiterate nation that angered them".
Kwa hiyo, utume na uteuzi ulihamishiwa kwa taifa la Waarabu lililodharauliwa, "lile jiwe ambalo wajenzi waliliacha limekuwa jiwe kuu la pembeni".
Therefore, the prophet-hood and the choice were transferred to the despised Arab nation "the brick which the builders refused became the corner stone".
Maandiko ya Injili na ya Torati yalitaja jina la Nabii na sifa zake, kwani Yesu (Amani iwe juu yake) alimwita "Paraklito", ambalo lina maana ya Ahmad, na malaika waliahidi kumhusu yeye: "na utii uko duniani, na Ahmad kwa watu" (kwa mujibu wa tafsiri ya kasisi wa zamani Abdul Ahad Dawood).
The Gospels’ and the Torah’s texts mentioned the name of the prophet and his characteristics, as Jesus (PBUH) called him "The Parakletos", which means Ahmad, and the angels promised of him "and the submission is on earth, and Ahmad to the people" (according to the translation of the previous priest Abdul Ahad Dawood).
Maandiko pia yalizungumzia nchi ambayo yeye atahama kwenda: "ufunuo kutoka upande wa nchi ya Waarabu, jangwani mwa nchi ya Waarabu", na yakatoa wito wa kumsaidia na kumhurumia yeye: "Enyi wakazi wa nchi ya Tema, mletee mkimbizi mkate wake" ﷺ.
The scriptures also talked about the land in which he will immigrate to "revelation from the side of the Arab land, in the wilderness of the Arab land", and called on supporting and sympathizing with him "O you residents of the Temaa land provide the fugitive with his bread".
Ilizungumzia pia ushindi wa nabii huyu, kwamba dini yake itafika duniani kote. Ndiye yule ambaye "mkono wake uko juu ya kila mtu, kwake mataifa yatanyenyekea, mataifa yaliyo chini yako yanaanguka, Atahukumu kati ya wapagani, atajaza mahali kwa maiti; atajeruhi vichwa katika nchi nyingi, wala hatachoka wala kudhoofika mpaka aiweke haki duniani.
It also talked about the victory of this prophet, that his religion will reach the whole world. He is the one that "his hand is on everyone, to him nations will submit, nations under you are falling, He shall judge among the heathen, he shall fill the places with the dead bodies; he shall wound the heads over many countries, and He shall not be tired or weak until he put the truth to the world.
Yeye ndiye ghadhabu inayowajia makafiri, kama Mayahudi ambao Yohana Mbatizaji aliwaonya. Akisema, "Enyi kizazi cha nyoka, ni nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu itakayokuja?… Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Uwanja wake wa kupepetea mikononi mwake, naye atasafisha kabisa sakafu yake, na kukusanya ngano yake ghalani; lakini atateketeza makapi kwa moto usiozimika."; na, "Kila atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjika; lakini juu ya yeyote litakapomwangukia, litamsaga kuwa unga."
He is the wrath that comes to the unbelievers, such as the Jews whom John the Baptist warned. Saying, "O generation of vipers, who hath warned you to flee from the wrath to come?… he shall baptize you with the Holy Ghost, and with fire. Whose fan is in his hand, and he will throughly purge his floor, and gather his wheat into the garner. but he will burn up the chaff with unquenchable fire.", and "Whosoever shall fall upon that stone shall be broken; but on whomsoever it shall fall, it will grind him to powder. ".
Tumeona pia kwamba manabii walitaja kwamba nabii huyu atakayekuja ndiye nabii wa mwisho na wa kufunga. Kwamba, ufalme wake, yaani sheria yake, utadumu milele. "Mungu wa mbinguni atasimamisha ufalme ambao hautaharibika kamwe … na utadumu milele", na "Lakini watakatifu walio juu watapokea ufalme, nao wataumiliki ufalme huo milele na milele". Muhammad ﷺ alisema, "Kundi la wafuasi wangu litabaki imara mpaka mapenzi ya Mungu yatakapokuja," na katika riwaya ya Muslim: (mpaka siku ya kiyama)1. Na yeye ndiye ambaye Yesu alimtabiri kwa taifa lake alipose: "Atawapa Mfariji mwingine ili akae nanyi milele".
We have seen also, that the prophets had mentioned that this coming prophet is the last and final prophet. That, his kingdom, meaning his statute, will last forever. "The Lord of heavens establishes a kingdom that will never Extinct … and it will stay forever", and "as for the upper saints they will take the kingdom, and they will keep the kingdom for eternity and forever". Muhammad (PBUH) said, “a group of my followers will remain steady until God’s will comes.), and in Muslim's narration: (until judgment day) 1, and that he is the one that Jesus (PBUH) prophesized to his nation when he said: “He will give you another Comforter to stay with you forever".
Ujumbe wa nabii huyu haukuwa mahsusi kwa Waarabu wala kwa wana wa Israeli, bali ni kwa mataifa yote, kama vile yeye "anailaumu dunia kwa dhambi" na "kwake mataifa yatanyenyekea", na yeye ndiye "matamanio ya mataifa yote", yule ambaye "kwa ajili ya mataifa yote, dola zote na lugha zote kuabudu".
The message of this prophet is not exclusive of the Arabs or the children of Israel, instead it is for all nations, as, he "blames the world for a sin" and "to him nations will submit", and he is "the desire of all nations", the one "for all nations, states and tongues to worship".
Zaidi, yeye ndiye Nabii asiyejua kusoma na kuandika ambaye Torati na Injili zilimweleza. "Nami nitaweka maneno yangu kinywani mwake", na yeye ndiye asiyejua kusoma na kuandika, ambaye utume wake ulitabiriwa katika pango la Hiraa. "Kisha kitabu hupewa yule asiyejua kusoma, akiambiwa, Soma hiki, nakusihi; naye husema, Mimi sijui kusoma."
Moreover, he is the illiterate prophet whom the Torah and the Gospels described. "and I will put my words in his mouth", and he is the illiterate, who was prophesized with the prophet-hood in the cave of Hiraa "And the book is delivered to him that is not learned, saying, Read this, I pray thee: and he saith, I am not learned.".
Yeye ndiye asiyezungumza kwa matamanio yake mwenyewe "hasemi kwa matamanio yake. Hayo si chochote isipokuwa ni ufunuo unaoteremshwa", na atafikisha ujumbe wake wote, na kifo au mauaji hayatasimama kinyume na utume wake "basi awaambie kila alichoamrishwa".
He is the one who does not speak from his own desire "does speak not from himself, but all what he hears he speaks with", and he will deliver all his message, and death or murder will not stand against his mission "so he speaks to them with all what I command him with".
Kama Musa (AS), yeye ana sheria "na visiwa vitangojea sheria yake." Na sheria yake inaungwa mkono kwa nguvu "na kutoka mkono wake wa kulia ikatoka sheria ya moto kwao." Sheria yake inajumuisha vipengele vyote vya maisha kwani yeye "anakufundisha kila kitu," na "anakuongoza kwenye kweli yote," na kwa kuja kwake Sheria ya Musa itafutwa: "Fimbo ya enzi haitaondoka kwa Yuda, wala mtawala wa sheria kutoka kati ya miguu yake, hata atakapokuja Shilo;" Yeye ndiye kiumbe mkuu zaidi, ilhali wanawake hawakumzaa mtu kama Yohana Mbatizaji, lakini "hata yule aliye mdogo zaidi katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye."
Like Moses (PBUH), he has a statute "and the isles shall wait for his law.", and his law is supported by strength "and from his right hand went a fiery law for them.” His law is comprehensive of all the aspects of life as he "teaches you everything", and "he guides you to all the truth", and with his appearance the Law of Moses will be abolished "The scepter shall not depart from Judah, nor a lawgiver from between his feet, until Shiloh come;" He is the greatest being, while women did not give birth to someone such as John the Baptist, but "notwithstanding he that is least in the kingdom of heaven is greater than he." (PBUH)
Christopher Davis, profesa wa dini linganishi, alikuwa sahihi aliposema, "Hakika unabii wote huu pamoja na maana na maelezo yake haulingani na mtu yeyote isipokuwa Nabii wa Kiarabu Muhammad ﷺ."
Christopher Davis, a professor of comparative religion, was right when he said, "Indeed, all these prophecies with it is meanings and descriptions does not match anyone except the Arabian prophet Muhammad (PBUH).
Vyanzo na Marejeo:
Sources and References:
Qur'an Tukufu
•The Holy Quran
• Biblia Takatifu, Toleo la English Standard Version.1981
• The Holy Bible, English Standard Version.1981
• Biblia Takatifu, Toleo la Biblia Takatifu ya Mashariki ya Kati, nakala ya Waprotestanti
• The Holy Bible, The Middle East Holy Bible’s publishers edition, Protestant’s copy
• Biblia Takatifu, Toleo la Wachapishaji wa Middle East, nakala ya Kiorthodoksi
• The Holy Bible, The Middle East Holy Bible’s publishers edition, Orthodox’ copy
• Biblia Takatifu, toleo la Ukuhani wa Wajesuiti, nakala ya Wakatoliki, iliyotolewa na Mapadre Wajesuiti, na kusambazwa na mashirika ya Biblia Takatifu Mashariki, Beirut. (Imetafsiriwa kutoka Good News Bible, Today's English Version, toleo la 2 la 1992)
• The Holy Bible, the Jesuit priest hood edition, Catholic’s copy, issued by the Jesuit fathers, and distributed by the Holy Bible's organizations in the East, Beirut. (Translated from the Good News Bible, Today’s English Version, 2nd Edition 1992)
• Biblia katika Kiingereza Rahisi (Basic English), 1965
• The Bible in Basic English, 1965
• Biblia ya Douay-Rheims, 1899
• Douay-Rheims Bible, 1899
• Biblia ya Darby, 1889
• Darby Bible, 1889
Biblia Takatifu (Maandiko Matakatifu ya Kiebrania na Maandiko Matakatifu ya Kigiriki) Tafsiri ya Ulimwengu Mpya, (toleo la Mashahidi wa Yehova)
• The Holy Bible (The Hebrew Holy Scriptures and the Greek Holy Scriptures) new world translation, (Jehovah witnesses’ edition)
• Torati ya Wasamaria, Imetafsiriwa na Padri Abu Al Hassan Isaac Assory, Imechapishwa na Ahmad Hijazy Al Saqa (toleo la kwanza)
• The Samaritan Torah, Translated by Priest Abu Al Hassan Isaac Assory, Published by Ahmad Hijazy Al Saqa (1st edition)
Al Ansar publishing, Cairo, 1398 lunar calendar
Al Ansar publishing, Cairo, 1398 lunar calendar
• Injili ya Barnaba, Tafsiri ya Khalil Saada. Toleo la Al Wathaeq Publishing. Kuwait, mwaka 1406 wa kalenda ya Kiislamu (Hijria), ------------------------------------------------------------------------------------------