4 Maisha ya Faragha
4 Private Life
Asili ya binadamu ni kwamba anaishi maisha ya hadharani na maisha ya faragha. Katika maisha ya hadharani anaishi pamoja na wanajamii katika kabila lake, kijiji chake au mji wake. Katika maisha yake ya faragha anaishi nyumbani kwake na miongoni mwa wanafamilia wake. Kwa ajili ya maisha yake ya faragha, Uislamu umeweka kanuni maalum za kushughulikia matatizo yanayomkabili binadamu, mwanamume au mwanamke. Mojawapo ya kanuni kuu ambazo Uislamu umeleta ni kwamba maisha ya faragha yako chini ya udhibiti wa binadamu huyo peke yake. Umekataza mtu yeyote kuingia nyumbani kwake bila ruhusa yake. Allah (SWT) anasema:
The nature of the human is that He lives a public and a private life. In public life He lives with members of society in his tribe, village or city. In his private life He lives at home and among his family members. For his private life, Islam introduced specific rules to treat the problems that the human encounters, male or female. One of the main rules that Islam brought is that the private life is exclusively under the control of that human. It forbade anyone to enter his house without his permission. Allah (swt) says:
“Enyi mlioamini, msiingie majumba yasiyokuwa yenu mpaka mpate idhini na kuwasalimia wakazi wake. Hilo ni bora kwenu, ili mpate kukumbuka.” [] Katika Aya hii, Allah (SWT) ameamuru watu wasiingie majumbani ambayo si yao bila ruhusa. Yeye (SWT) amezingatia kutoomba ruhusa kuwa ni kutokujuana, na kuomba ruhusa kuwa ni kujuana. Amesema: