Haqaa'iq (Ukweli) na Abaateel (Uongo):
Haqaa’iq (truths) and Abaateel (Falsehoods):
Madhalimu na wafuasi wao wanaogopa Ummah kuongozwa kwenye njia sahihi ya mabadiliko na kufufuka. Hili ni onyo kwao kuhusu mwisho wa upotovu wao, dhulma yao na udanganyifu wao. Kwa hiyo jambo lao la msingi ni kushughulika na kuwamaliza wale wanaowalingania kwenye Haqq. Kwa hiyo, baada ya kuiangamiza Dola ya Kiislamu, waliyararua mataifa na kuyabadilisha kuwa dola ndogo nyingi, wakaweka mawakala wao waaminifu katika nafasi za mamlaka ndani yake. Baada ya hapo wakachukua hatua za kisiasa ambapo waliwapandisha mawakala wao, wakiwawasilisha kama mashujaa na viongozi wa ukombozi na kufufuka, huku wakikandamiza vikali kila harakati na kila vuguvugu lililokuwa la dhati.
The tyrants and their supporters are frightened of the Ummah being guided to the correct path towards change and revival. This represents a warning to them in respect to the end of their falsehood, oppression and deception. As such it is their vital issue to deal with and put an end to those who are inviting to the Haqq. Therefore after they destroyed the Islamic State, tore up the lands and replaced them with many small statelets and placed their loyal agents in the positions of authority within them. After that they undertook political actions in which they promoted their agents presenting them as heroes and the leaders of liberation and revival whilst vehemently suppressing every action and movement which was sincere.
Mawakala na watumishi hao waaminifu walishirikiana na mabwana zao kuwapotosha na kuwadanganya Ummah kwa lengo la kumaliza Uislamu kwa kiwango kinachozidi kuongezeka. Kwa sababu hiyo, vyama vingi vya kisekula na vya kikomunisti vilizuka, huku Da'wah ya Kiislamu ikizuiwa na kukatazwa, isipokuwa aina zile zilizolenga kuwaweka watu mbali na kazi ya kweli na sahihi iliyotumikia malengo ya udanganyifu na kuwapotosha zaidi watu. Kufuru ilipewa jina la Uislamu, mawazo ya Uislamu yanayohusiana na utawala na siasa yalifutwa, huku hukumu za Kiislamu zinazohusiana na mbinu zikifutiliwa mbali kiasi kwamba Uislamu ukawa kitu cha ajabu miongoni mwa watu wake wenyewe.
Those agents and loyal servants worked alongside their masters to increasingly mislead and deceive the Ummah with the objective of finishing of Islaam. As such many secular and communist parties arose whilst the Islaamic Da’wah was prevented and forbidden apart from the forms that aimed at distancing people from the sincere and correct work which served the aims of deception and further mislead the people. Kufr was then presented with the name of Islaam, the thoughts of Islaam related to ruling and politics were made absent whilst the Islamic rulings related to the method were wiped out to the point that Islaam became something strange amongst its own people.
Ummah ya Kiislamu iligeuka kuwa mataifa yenye chuki na uhasama wa pande zote. Mshikamano wa kitaifa na wa kizalendo ulijitokeza na kuibuka. Kila taifa au dola ndogo ilikuwa na mfumo au suala lililopingana na tofauti na lile la jingine. Masuala ya tofauti na mzozo yalichochewa, wakati dola ya Kiyahudi ilipandikizwa kama kisu chenye sumu moyoni mwa Ummah.
The Islamic Ummah became States with mutual hatred and resentment between each other. The nationalistic and patriotic allegiances manifested and arose, every State or Statelet had a System or issue which was contrary and different from the other, the issues of difference and dispute were incited whilst the Jewish State was planted as a dagger in the very heart of the Ummah.
Kwa kuwa Uislamu ni Aqeedah na Shariy'ah ambayo Ummah yote kwa jumla inaiamini, kafiri na mawakala wake hujaribu kuipotosha Ummah katika fikra na maoni yake mengi. Miongoni mwa hayo ni fikra kwamba Uislamu hauna nafasi yoyote katika siasa, kwamba umoja wa Ummah ni jambo lisilowezekana kiutendaji, na hata kwamba kusimamishwa kwa Khilafah pia ni jambo lililo nje ya uwezekano wote.
Because Islaam is an Aqeedah and Sharee’ah which the Ummah in its entirety believes in, the disbeliever and his agents attempt to mislead the Ummah in many of her thoughts and opinions. These included the thought that Islaam has no say in politics, that the unity of the Ummah is an impractical matter and indeed impossible, and that the establishment of the Khilafah was also a matter that was beyond all possibility.
Reference: Taghyeer (mabadiliko) - Mahmoud Abdul-Kareem Hasan