5.6 Kuhesabu Mafanikio na Kushindwa
5.6 Accounting For Success And Failure
Pamoja na ongezeko la mikopo katika kipindi hiki, tumeshuhudia pia kudorora kwa viwango vya uhasibu ambavyo vimechangia kutokuwa na uhakika na kupungua kwa imani katika mfumo kwa ujumla. Sambamba na ukuaji wa mikopo kumekuwa na ongezeko la uwekaji wa mali na madeni "nje ya mizania" (off-balance sheet), mengi yakiwa ni bidhaa zinazotokana na mikataba ya kifedha (derivatives). Hali hii imewezesha kushikilia mali na madeni hatarishi bila kuonekana na wawekezaji na wasimamizi wa sekta. Ukubwa wa jambo hili unaonekana katika benki ya Citigroup, iliyosaidiwa hivi karibuni kifedha na ambayo ndiyo benki kubwa zaidi duniani. Ilipofika Juni 2008, Citigroup ilikuwa na mali na madeni nje ya mizania yenye thamani ya dola trilioni 1.2. Pauline Wallace, mshirika wa kampuni ya PriceWaterhouseCoopers LLP, alieleza kwa usahihi uhasibu huu wa nje ya mizania alipokuwa akisema: "Wachawi huja kwenye karamu, nao hufanya vitu vionekane vinapotea. Hatari ipo mahali fulani, lakini haujui kamwe ilipo28".
Along with the run up in credit over this past period we have seen a deterioration in accounting standards that have contributed to uncertainty and a lack of confidence in the system in general. Mirroring the growth in credit has been a growth in “off-balance sheet” recording of assets and liabilities, many of which are derivatives. This has enabled the holding of risky assets and liabilities beyond the gaze of investors and regulators alike. The extent of this could be seen in the recently bailed out Citigroup, the largest bank in the world, which as of June 2008 had 1.2 Trillion dollars of off-balance sheet holdings. Pauline Wallace, a partner at PriceWaterhouseCoopers LLP accurately portrayed this off-balance sheet accounting when she said: “Magicians come to parties, and they make things seem to disappear. The risk is somewhere, but you never knew where28”.