8. Hizb ut-Tahrir
8. Hizb Ut-tahrir
Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislamu cha kimataifa, kilichoanzishwa mwaka 1953 chini ya uongozi wa mwanzilishi wake, msomi, mwanafikra wa kisiasa na jaji katika Mahakama ya Rufaa huko al-Quds (Yerusalemu), Taqiuddin an-Nabhani. Uongozi wa kimataifa wa Hizb ut-Tahrir kwa sasa unaongozwa na Ata’ abu Rishta. Katika ulimwengu wa Kiislamu, Hizb ut-Tahrir inafanya kazi katika ngazi zote za jamii ili kuwarudisha Waislamu kwenye kuishi maisha ya Kiislamu chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah (Ukhalifa), kwa kufuata mbinu ya kisiasa pekee.
Hizb ut-Tahrir is a global Islamic political party that was established in 1953 under the leadership of its founder - the scholar, political thinker and judge in the Court of Appeals in al-Quds (Jerusalem), Taqiuddin an-Nabhani. Hizb ut-Tahrir global leadership is currently headed by Ata’ abu Rishta. In the Muslim world, Hizb ut-Tahrir works at all levels of society to bring the Muslims back to living an Islamic way of life under the shade of the Khilafah (Caliphate) State following an exclusively political method.
Hizb ut-Tahrir inachukua mbinu iliyotumiwa na Mtume Muhammad ﷺ alipoanzisha Dola ya kwanza ya Kiislamu huko Madina. Mtume Muhammad ﷺ alijizuia katika juhudi zake za kuanzisha Dola ya Kiislamu kwa kazi ya kifikra na kisiasa pekee. Alianzisha dola hii ya Kiislamu bila kutumia nguvu wala vurugu. Alifanya kazi ya kuhamasisha maoni ya umma kuunga mkono Uislamu, na alijitahidi kuwashawishi wasomi wa kisiasa na kifikra wa wakati ule. Licha ya mateso naususiaji aliopata Mtume Muhammad ﷺ pamoja na Waislamu wa mwanzo, hawakuwahi kutumia vurugu. Kwa hiyo chama kinajishughulisha kikamilifu katika kueneza mawazo ya Kiislamu ya kifikra na kisiasa kwa upana katika jamii za Waislamu, ili kupinga hali iliyopo sasa katika jamii hizo. Chama kinaiwasilisha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha unaoweza kusimamia mambo ya dola na jamii. Chama pia kinatoa maoni yake kuhusu matukio ya kisiasa na kuyachambua kwa mtazamo wa Kiislamu.
Hizb ut-Tahrir adopts the methodology employed by the Prophet Muhammad (peace be upon him) when he established the first Islamic State in Madinah. The Prophet Muhammad limited his struggle for the establishment of the Islamic State to intellectual and political work. He established this Islamic state without resorting to violence. He worked to mobilise public opinion in favour of Islam and endeavoured to sway the political and intellectual elites of the time. Despite the persecution and boycott of the Prophet Muhammad and the early Muslims, they never resorted to violence. The party is therefore proactive in disseminating the Islamic intellectual and political thoughts widely in Muslim societies so as to challenge the existing status quo that exists there. The party presents Islam as a comprehensive way of life that is capable of managing the affairs of state and society. The party also expresses its views on political events and analyses them from an Islamic perspective.
Chama hiki kinasambaza mawazo yake kupitia mazungumzo na umma, halaqa za masomo, mihadhara, semina, usambazaji wa vipeperushi, uchapishaji wa vitabu na majarida, na kupitia mtandao wa Intaneti. Tunawahimiza watu kuhudhuria maandamano yetu, matembezi ya kuandamana na mikesha yetu.
The party disseminates its thoughts through discussion with the masses, study circles, lectures, seminars, leaflet distribution, publishing books and magazines and via the Internet. We encourage people to attend our demonstrations, marches and vigils.
Katika nchi za Magharibi, Hizb ut-Tahrir inajitahidi kulea jamii ya Waislamu inayoishi kwa Uislamu katika fikra na matendo, ikizingatia kanuni za Uislamu na kuhifadhi utambulisho thabiti wa Kiislamu. Chama hakifanyi kazi nchini Magharibi kwa lengo la kubadilisha mfumo wa serikali. Pia chama kinajitahidi kuonyesha picha chanya ya Uislamu kwa jamii ya Magharibi na kushiriki mazungumzo na wanafikra wa Magharibi, watunga sera na wasomi. Serikali za Magharibi, chini ya bendera ya Vita dhidi ya Ugaidi, kwa sasa zinafanya juhudi za kuuwasilisha Uislamu kama 'itikadiovu'. Kwa kweli, kiini cha kampeni hii ni kuchafua itikadi ya Kiislamu kama mbadala wa ubepari huria wa Magharibi. Kwa sababu ya upande huu wa propaganda katika Vita dhidi ya Ugaidi, Hizb ut-Tahrir inajitahidi kujenga maoni kuhusu Uislamu katika nchi za Magharibi, kama imani, itikadi na mbadala kwa ulimwengu wa Kiislamu.
In the West, Hizb ut-Tahrir works to cultivate a Muslim community that lives by Islam in thought and deed, adhering to the rules of Islam and preserving a strong Islamic identity. The party does not work in the West to change the system of government. The party also works to project a positive image of Islam to Western society and engages in dialogue with Western thinkers, policymakers and academics. Western governments, under the banner of the War on Terror, are currently working to present Islam as an ‘evil ideology’. Indeed at the heart of this campaign is to malign the Islamic ideology as an alternative to Western liberal capitalism. Because of this propaganda aspect to the War on Terror, Hizb ut-Tahrir works to develop opinion about Islam in the Western countries, as a belief, ideology and alternative for the Muslim world.