5.2 Mifano ya Ijma‟ as-Sahabah
5.2 Examples of Ijma‟ as-Sahabah
Mfano wa Ijma‟ as-Sahaba ni kipaumbele kinachopaswa kutolewa katika kumteua Khalifa wa Waislamu. Sunnah ya Mtume ﷺ inatufahamisha kwamba maiti lazima azikwe haraka, na ni haramu kwa wale wanaohusika na mazishi kuchelewesha mazishi kwa sababu ya mambo mengine. Hata hivyo, Mtume ﷺ alipofariki, Maswahaba walichelewesha mazishi yake ﷺ hadi walipomchagua Khalifa miongoni mwao.
An example of Ijma‟ as-Sahabah is the priority, which must be given to the appointment of a Khaleefah for Muslims. The Sunnah of the Prophet (saw) informs us that the dead must be buried quickly and it is forbidden for those responsible for the burial to delay the burial on account of other things. Yet when the Prophet (saw) died, the Companions delayed his (saw) burial until they had selected a Khaleefah from among themselves.
Kabla ya kukamilisha mipango ya mazishi, Maswahaba (ra) walikusanyika katika eneo la Banu Sai‟da na kuendelea kumchagua Khalifa. Baada ya majadiliano juu ya jambo hilo, wote walikubaliana kumpa Bay‟ah (kiapo cha utii) Abu Bakr (ra), baada ya hapo wakamzika Mtume ﷺ. Hakuna hata mmoja wao aliyepinga kuchelewa kwa mazishi. Makubaliano ya pamoja ya Maswahaba (ra) kuhusu kitendo hiki ni dalili kwetu juu ya umuhimu wa kuteua Khalifa wa Waislamu, hata muhimu zaidi kuliko mazishi ya Mtume ﷺ mwenyewe.