1.4 Njia Ya Tafsiri
1.4 The Method Of Tafseer
Qur'aan ni kitabu cha mwisho cha wahyi wa Mwenyezi Mungu kilichoteremshwa kwa binadamu, na Allaah ameahidi kukilinda dhidi ya upotoshaji wowote au upotevu. Amesema katika Qur'aan:
The Qur’aan is the last book of divine revelation sent to man, and Allaah has promised to protect it from any distortion or loss. He said in the Qur’aan:
Hakika Sisi tumeiteremsha Ukumbusho (Qur-aan), na hakika Sisi ndio tutaolinda.” 65
“Verily, I have revealed the Reminder (Qur’aan) and verily I will preserve it.” 65
Maandiko yake yaliyoandikwa na yanayosomwa yamehifadhiwa bila mabadiliko hata kidogo kwa zaidi ya miaka elfu moja mia nne, kama ilivyotajwa katika sura zilizopita. Hili haliwezi kusemwa kuhusu Injili ya Nabii Isa (r), wala vitabu vya Agano la Kale vinavyohusishwa na manabii waliotangulia, wala kitabu chochote kingine cha wahyi alichoteremsha Allah. Hata hivyo, ulinzi wa Allah juu ya Qur'an haukuishia hapo; Yeye pia alilinda maana yake halisi. Kama ulinzi wa maana ya Qur'an usingetokea, wapotofu wangeigeuza Kitabu cha Allah kuwa mkusanyiko wa alama, vitendawili na misimbo inayoweza kutafsiriwa kwa namna nyingi, na maana yake ya asili ingepotea. Allah alihifadhi maana ya Qur'an kwa kufafanua baadhi ya mambo yake ya jumla ndani ya Qur'an yenyewe, na kwa kumkabidhi Mtume Wake, Muhammad bin Abdillah ﷺ (570-632 BK), tafsiri ya mengineyo.