4.8 Muujiza ya Kihesabu ya Qur'aan
4.8 The Numerical Miracle of the Qur’aan
Mtetezi maarufu wa wazo hili alikuwa Rashad Khalifa, mwanakemia wa viumbe hai (biokemia) raia wa Misri aliyesomea nchini Marekani. Kwa mujibu wa Dkt. Khalifa, kuna msimbo wa kihesabu wa ajabu katika Qur'ani unaotokana na aya yake ya "kwanza" (BismillahirRahmaanir-Raheem), ambayo ina herufi 19. Msimbo huu wa ajabu unadaiwa kutajwa katika aya ya 30 ya Sura ya 74 (al-Muddath-thir) inayosema "Juu yake kuna 19." Kwa kutegemea mambo haya mawili, Dkt. Rashad anadai kugundua muundo tata wa kihesabu unaohusisha namba 19 na mazidisho yake katika Qur'ani yote, na hasa katika kile alichokiita herufi za mwanzo za Qur'ani, zinazotangulia sura 29 (Alif, Laam, Meem, n.k.). Kutokana na ugunduzi huu, Dkt. Khalifa anahitimisha kwamba utata wa muundo wa msimbo huu wa kihesabu katika kazi ya kifasihi yenye ukubwa wa Qur'ani uko mbali sana zaidi ya uwezo wa binadamu, na kwamba peke yake ndio muujiza halisi wa Qur'ani unaothibitisha asili yake ya kimungu. Pia anahitimisha kwamba 19 na mazidisho yake ndiyo ufunguo wa tafsiri sahihi ya Qur'ani na Uislamu, na kwamba sababu ya kuchaguliwa kwa 19 ni kwamba 19 ina maana ya "Mungu ni Mmoja," ambalo ndilo ujumbe wa Qur'ani.81