7.3 Enzi ya ‘Uthmaan 644-656 CE/23-35 AH
7.3 The Era Of ‘uthmaan 644-656 Ce/23-35 Ah
Baada ya kifo cha khalifa wa pili, ‘Umar ibn al-Khattaab, kamati iliyoundwa na masahaba sita maarufu zaidi wa Mtume ﷺ ilimchagua ‘Uthmaan ibn ‘Affaan kuwa khalifa wa tatu.
After the death of the second Caliph, ‘Umar ibn al-Khattaab, a committee made up of six of the most famous companions of the Prophet (r) chose ‘Uthmaan ibn ‘Affaan to be the third caliph.
Wakati wa utawala wa Khalifa ‘Umar (634-644 CE/13-23 AH), dola ya Kiislamu ilikuwa imepanuka zaidi ya mipaka ya Rasi ya Arabia hadi Misri, Shamu na ‘Iraq. Katika utawala uliofuata wa Khalifa ‘Uthmaan, upanuzi uliendelea hadi Uajemi, India, Urusi, China, Uturuki na kuvuka Afrika Kaskazini. Watu wengi wa maeneo haya walikubali Uislamu na kujifunza usomaji wa Qur’aan kutoka kwa Waislamu wa mwanzo. Qur’aan ilishushwa kwa Nabii (ﷺ) kwa lahaja saba tofauti za Kiarabu, na Waislamu wa mwanzo walifundisha Qur’aan katika usomaji wake tofauti.
During the reign of Caliph ‘Umar (634-644 CE/13-23 AH), the Islaamic state had expanded beyond the borders of the Arabian peninsula into Egypt, Syria and ‘Iraaq. In the subsequent reign of Caliph ‘Uthmaan, the expansion continued on into Persia, India, Russia, China, Turkey and across North Africa. Many of the people of these regions accepted Islaam and learned the recitation of the Qur’aan from the early Muslims. The Qur’aan was revealed to the Prophet (ﷺ) in seven different Arabian dialects, and the early Muslims taught the Qur’aan in its different readings.