10 Da'wah Madinah
10 The Da’wah in Madinah
Watu wa kiapo cha kwanza cha al-‘Aqabah waliporejea Madina na Uislamu ukaenea katika kila nyumba miongoni mwa Answari, walimtuma mtu kwa Mjumbe wa Allah ﷺ kwa barua wakiomba amtumie mtu wa kuwafundisha Dini na Qur’ani. Mjumbe wa Allah ﷺ hakuwahi kuwaacha wale waliosilimu bila kuwafundisha hukumu na kuwalea kwa utamaduni safi wa Kiislamu utakaowawezesha kuelewa Uislamu na kutambua kiini chake. Kwani utamaduni wa Kiislamu ni muhimu kwa kila Muislamu, ni njia ya kuimarisha ‘Aqeedah na kuelewa Ujumbe wa Uislamu, na hivyo unahakikisha utekelezaji thabiti wa Uislamu. Wale waliosilimu walihisi hili, kwa hiyo wakaomba mtu wa kuwafundisha, na Mjumbe wa Allah ﷺ akamtuma Mus’ab bin ‘Umayr kwao.
When the people of the first pledge of al-‘Aqabah returned to Madinah and Islam spread to every single household among the Ansar, they sent a man to the Messenger of Allah (pbuh) with a letter asking him to send them someone who would teach them the Deen and the Qur’an. The Messenger of Allah (pbuh) never used to leave those who embraced Islam without teaching them the rules and nurturing them with the sound Islamic culture which would enable them to understand Islam and realize its essence. For the Islamic culture is vital to every Muslim, and is a means of strengthening the ‘Aqeedah and of understanding the Message of Islam, and thereby guarantees the consistent application of Islam. Those who embraced Islam had sensed this, therefore, they asked for someone to teach them, and the Messenger of Allah (pbuh) sent Mus’ab ibn ‘Umayr to them.