44 Uharibifu wa Dola ya Kiislamu
44 The Destruction of the Islamic State
Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano na washirika kupata ushindi mkubwa, Dola ya 'Uthmani iliangamizwa na kugawanywa vipande vidogo vidogo. Washirika waliteka ardhi zote za Kiarabu, Misri, Shamu, Palestina, Transjordan na Iraq, wakiziondoa kwenye Dola, hivyo kilichobaki mikononi mwa 'Uthmani ni Uturuki pekee, nayo yenyewe ilikuwa imevamiwa na washirika. Meli za kivita za Uingereza ziliteka Bosporus, na jeshi la Uingereza likaikalia sehemu za mji mkuu, Istanbul, pamoja na ngome zote za Dardanelles na maeneo mengi ya kimkakati kote Uturuki.
In the wake of the First World War, after a truce had been declared and once allies had secured their sweeping victory, the ‘Uthmani State was destroyed and fragmented into small statelets. The allies seized all the Arab lands, Egypt, Syria, Palestine, TransJordan and Iraq, stripping them from the State so that all that remained in the hands of the ‘Uthmanis was Turkey, and even she had been invaded by the allies. British warships seized the Bosporus and the British army occupied parts of the capital, Istanbul, all the Dardanelle fortresses, and most of the strategic points throughout the whole of Turkey.