Kuwaunda Watu Kuwa Umma Moja
37 Moulding People into One Ummah
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alifariki baada ya Rasi yote ya Uarabuni kuingia katika dini ya Kiislamu na ushirikina kuondolewa. Rasi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa Kiislamu, ikitawaliwa kikamilifu kwa Uislamu kulingana na ‘Aqeedah yake na mfumo uliotokana nayo. Alifariki ﷺ tu baada ya Mwenyezi Mungu (SWT) kukamilisha Dini, kutimiza neema yake kwa Waislamu, na kuwachagulia Uislamu kuwa dini yao. Hili lilijumuisha kuwalingania Uislamu mataifa na watu jirani kwa kuwatuma wajumbe kwa wafalme na watawala wao, pamoja na kutuma misafara ya kuvamia mipaka ya Warumi ya Mu’tah na Tabuk.
The Messenger of Allah (pbuh) passed away after the entire Arabian Peninsula had entered into the fold of Islam and polytheism had been abolished. The Peninsula was under the Islamic domain, ruled comprehensively by Islam according to its ‘Aqeedah and the system that emanated from it. He (pbuh) died only after Allah (swt) had perfected the Deen, completed His favor unto the Muslims and chose for them Islam as that Deen. This included the invitation of neighboring nations and people to Islam by sending envoys to their kings and rulers as well as by dispatching expeditions to raid the Roman frontiers of Mu’tah and Tabuk.