Jinsi Dola ya Kiislamu Ingeweza Kusimama
48 How the Islamic State Would Rise
Nguvu ya fikra ya Kiislamu pamoja na mbinu yake ingetosha kuanzisha Dola ya Kiislamu na kurejesha mfumo wa maisha wa Kiislamu, mradi tu fikra hii imekita mizizi katika nyoyo na akili za Waislamu, na kwamba imejidhihirisha kwa Waislamu katika nyanja zote za maisha. Hata hivyo, licha ya haya yote, kuna kazi kubwa mno ambazo lazima zifanywe kabla ya kuanzishwa upya kwa Dola, na juhudi za ajabu lazima zifanywe ili kurejesha mfumo wa maisha wa Kiislamu. Kwa hiyo, hamu na matumaini peke yake hayatatosha kwa Dola kusimama, wala hima na shauku haitatosha kuhakikisha kurejeshwa kwa mfumo wa maisha wa Kiislamu. Wajibu mama wa majukumu yote ni kupima kwa uangalifu vikwazo hivi vikubwa vinavyosimama kwenye njia ya Uislamu, ili kuweza kuviondoa.
The strength of the Islamic thought coupled with its methodology would be sufficient to establish the Islamic State and to resume the Islamic way of life, provided that this thought is deeply rooted in the hearts and minds of the Muslims, and that it materialized itself in the Muslims in all walks of life. However, despite all this, some colossal tasks have to be carried out prior to the reestablishment of the State, and phenomenal efforts must be made in order to resume the Islamic way of life. Desire and optimism would not, therefore, be sufficient for the State to arise, nor would hope and enthusiasm be enough to secure the resumption of the Islamic way of life. The mother of all duties would be to duly assess these colossal obstacles which stand in the way of Islam in order to make their removal possible.