40 Uvamizi wa Wamishonari
40 The Missionary Invasion
Ulaya ilianza uvamizi wake dhidi ya Dola ya Kiislamu kwa jina la sayansi, na ikatenga bajeti kubwa kwa madhumuni hayo. Kwa kweli, uvamizi huo ulikuwa wa kikoloni kwa siri, lakini ukajificha nyuma ya kazi ya umishonari kwa jina la sayansi na msaada wa kibinadamu. Uvamizi huu ulipangwa kuwezesha idara za ujasusi wa kisiasa na za ukoloni wa kitamaduni kujiweka katika nchi za Kiislamu hadi zikawa kiini na kikosi cha mbele cha mashine ya kikoloni ya Magharibi. Ukoloni ulianza pale ulimwengu wa Kiislamu ulipofungua milango yake kwa utamaduni wa Magharibi kupitia kivuli cha vyama vya umishonari, ambavyo vilikuwa hasa vya Kifaransa, Kiingereza na Kimarekani.
Europe began its invasion of the Islamic State in the name of science and it appropriated large budgets for that purpose. In fact, the invasion was covertly colonial, but disguised as missionary work in the name of science and humanitarian aid. This invasion was designed to enable the departments of political intelligence and cultural colonization to settle in Muslim countries until they became the heart and spearhead of the Western colonial juggernaut. Colonization began when the Muslim world opened its gates to Western culture via the guise of missionary associations, which were mainly French, English and American.