26 Ukombozi wa Makkah
26 Liberation of Makkah
Mara tu baada ya mkataba wa Hudaybiyah kutiwa saini kati ya Mjumbe wa Allah ﷺ na Quraysh, kabila la Khuza'ah likaingia chini ya ulinzi wa Mjumbe wa Allah ﷺ, na Banu Bakr wakajiunga upande wa Quraysh. Uhusiano kati ya Quraysh na Mjumbe wa Allah ﷺ ulibaki wa amani, na pande zote mbili zikaendelea tena na shughuli zao za kibiashara. Quraysh walipanua biashara yao ili kufidia yale waliyoyapoteza wakati wa vita dhidi ya Waislamu. Mjumbe wa Allah ﷺ aliendelea na kazi yake ya kuufikisha Ujumbe wa Uislamu kwa binadamu wote, huku akiimarisha pia nafasi ya Dola ya Kiislamu katika Rasi ya Arabia na kuhakikisha usalama ndani ya Dola yenyewe.
As soon as the treaty of Hudaybiyah was signed between the Messenger of Allah (pbuh) and the Quraysh, the tribe of Khuza’ah came under the protection of Allah’s Messenger (pbuh) and Banu Bakr sided with the Quraysh. Relations between the Quraysh and the Messenger of Allah (pbuh) remained peaceful and both sides resumed their business. The Quraysh expanded their trade in order to make up for what they had lost during the wars against the Muslims. Allah’s Messenger (pbuh) pursued his task of conveying the Message of Islam to the whole of mankind while simultaneously strengthening the position of the Islamic State over the Arabian Peninsula and providing safety and security within the State itself.