11.3 Taghut ni nini?
11.3 What Is Taghut?
Uislamu umeamua kwamba kurejea kwa mtu mwingine yeyote isipokuwa Allah kwa ajili ya hukumu ni kumrejea Twaghut. Yeye amesema: “Je, hukuwaona wale (wanafiki) wanaodai kwamba wanaamini yale yaliyoteremshwa kwako, na yale yaliyoteremshwa kabla yako, na wanataka kwenda kwa hukumu (katika mizozo yao) kwa Twaghut, ilhali wameamrishwa wayakatae?
Islam has determined that referring for judgment to anyone other than Allah constitutes referring to the Taghut. He said; “Have you seen those (hypocrites) who claim that they believe in that which has been sent down to you, and that which was sent down before you, and they wish to go for judgment (in their disputes) to the Taghut while they have been ordered to reject them.
Lakini Shaytani anataka kuwapoteza mbali sana.” [TMQ 4:60] Hukumu ya Ṭāghūt ni hukumu ya Jāhiliyyah. Ni kila hukumu inayopingana na hukumu ya Allah na ya Mtume wake . Ibn al-Qayyim anasema katika kitabu chake, A’laam al-muwaqqi’een: “Ṭāghūt ni kila kitu ambacho mja hupita mipaka kwacho, kwa upande wa kitu kinachoabudiwa, mtu anayefuatwa au kutiiwa. Hivyo, Ṭāghūt wa kila watu ni yule ambaye wanamrejea kwa hukumu badala ya Allah na Mtume Wake, au yule wanayemwabudu badala ya Allah, au wanayemfuata bila ushahidi kutoka kwa Allah, au wanayemtii katika yale wasiyojua kuwa ni katika utiifu kwa Allah.” Qur’ani inaona kuwa Imani ya mtu anayemrejea Ṭāghūt ni dai au kujifanya na si uhalisia. Pia Qur’ani imemfanya Ṭāghūt kuwa mpinzani wa Imani pale Yeye aliposeme: “Basi atakayemkataa Ṭāghūt na kumwamini Allah, basi amekamata kishikio kilicho imara zaidi.” [TMQ 2:256] Hivyo, Umma wa Kiislamu lazima uwe shahidi juu ya wanadamu baada ya Mtume hadi Siku ya Kiyama. Umma unapaswa kuwaambia wanadamu yale ambayo Qur’ani imeyasema: “Mwabuduni Allah (peke yake), na jiepusheni (au kujitenga mbali) na Ṭāghūt.” [TMQ 16:36] Kwa hiyo, wazo la kutenganisha dini na maisha, na mawazo yanayotokana nalo, kama Demokrasia, ni mawazo ya Ṭāghūt. Uislamu umetuamuru tuyatupilie mbali na tuyakatae.
But Shaytan wishes to lead them far astray.” [TMQ 4:60] The rule of Taghut is the rule of Jahiliyyah. It is every rule that contradicts the rule of Allah and His Messenger . Ibn al-Qayyim says in his book, A’laam al-muwaqqi’een; “Taghut is everything with which the servant exceeds the bounds, in terms of something that is worshipped, someone followed or obeyed. Thus, the Taghut of every people is the one whom they refer to for judgment other than Allah and His Messenger, or the one they worship other than Allah, or follow without a proof from Allah, or obey in what they do not know as being from the obedience to Allah.” The Qur’an considers the Imaan of the one who refers to Taghut as a claim or pretense and not a reality. Also the Qur’an has made Taghut a rival to Imaan when He said; “Whoever disbelieves in Taghut and believes in Allah, then he has grasped the most trustworthy handhold.” [TMQ 2:256] Thus, the Islamic Ummah must be a witness over mankind after the Messenger until the Day of Judgment. The Ummah should say to mankind what the Qur’an has said; “Worship Allah (alone), and avoid (or keep away from) Taghut.” [TMQ 16:36] Therefore, the idea of separating religion from life, and the thoughts that emanate from it, such as Democracy, are thoughts of Taghut. Islam has commanded us to discard and reject them.
Hii ni Demokrasia, na hii ndiyo maoni ya Uislamu kuhusu hilo. Kuhusu matokeo yanayozalishwa kwa kutekeleza yote haya duniani, je, ni mfumo wenye heshima na uzuri ambao tungependa kuishi chini yake, au ni mfumo mbaya, unaowaunguza watu kwa moto wake huku wakiishi maisha ya utupu na hasara kutokana na utekelezaji wake?
This is Democracy and this is the opinion of Islam regarding it. As for the results produced by applying all of this on the earth, is it an honorable and beautiful system under which we would like to live or is it an evil system, which burns the people with its fire whilst they live a life of emptiness and loss due to its application?