4.7 Kutafuta Nusrah (Msaada wa Kimali)
4.7 Seeking The Nusrah (material Support)
Tuchunguze kwa muda sheria muhimu miongoni mwa sheria za mbinu hii, yaani kutafuta Nusrah. Tuichunguze tena polepole ili tupate kuelewa tunachopaswa kufuata, hasa kwa kuwa kuna watu wanaofanya kazi ya kuanzisha Dola ya Kiislamu, lakini hawaitilii Nusrah umakini hata kidogo. Wanaitendea kana kwamba ni jambo la pembeni lisilo na uzito, au kana kwamba mnyororo wa wapokezi (isnad) wake ni dhaifu, hivyo haipaswi kuchukuliwa. Hawakuishia hapo, bali waliendelea kuishambulia sheria hii na wale waliojishughulisha nayo, ilhali wasifu wote wa Mtume ﷺ umezungumzia somo hili, kukiwa na tofauti ndogo chache katika maelezo, ambazo hazistahili kutajwa. Waandishi wa Sirah hawakuwa wanachama wa mojawapo ya makundi tunayoyajua leo, lakini licha ya hayo walijadili somo hili. Qur'ani yenyewe imewataja wale ambao; "walitoa msaada" [TMQ 8:72], na kuwaita "Ansaar (Wasaidizi)" [TMQ 9:100]. Ni maelezo ya sifa njema na maelezo ya jambo lililo maarufu zaidi kwa sifa ambazo walitambulika nazo.
Let us consider for a while an important rule from the rules of the method, that is, the seeking of the Nusrah. Let us slowly re-examine it so as to deduce what we need to follow, especially since there are people who are working to establish the Islamic State, but do not give the Nusrah the slightest attention. They do this as if it is a periphiral matter, which carries no weight, or as if its isnad (chain of narration) is weak, and so should not be taken. They did not stop here, but went on to attack this rule and those who engaged in it, even though all the biographies of the Prophet addressed this subject, with only a few minor differences in the details, which are not worth mentioning. The authors of the Sirah were not affiliated to any of the groups we know today, but despite this they discussed this subject. The Qur’an itself has mentioned those who; “gave help” [TMQ 8:72], and called them the, “Ansaar (Helpers)” [TMQ 9:100]. It is a description of praise and a description of the most prominent aspect by which they were characterised.