5. Mbinu Zinazopingana na Njia ya Kishari'a
5. Methods Contrary To The Shar’ee Method
Ikilinganishwa na yale tuliyoyataja kuhusu mwenendo wa Mtume ﷺ na umuhimu wa kumfuata na kutokupotoka kutoka kwake, tunaona kuna mbinu nyingine zilizochukuliwa na makundi ya Kiislamu au wasomi wa Kiislamu, ambazo zinahusiana na somo hili. Bila kujali aliyeyasema, sharti tushughulikie yale yaliyosemwa. Ni lazima tuyapitie kwa ufupi, tukiondoa pazia kutoka kwake, ili Muislamu asiendelee kuchanganyikiwa na kupotea katika mtego wa mbinu hizi, au kuingiwa na shaka kuhusu kubeba da'wah. Katika yanayofuata, tunawasilisha baadhi ya mbinu muhimu zaidi.
As compared with what we have mentioned about the method of the Messenger and the importance of emulating it and not deviating away from it, we find there are other approaches adopted by Islamic groups or Muslim intellectuals, which relate to this subject. Regardless of who said it, we must concern ourselves with what has been said. We must undertake a quick examinination of them, removing the veil from them, so that the Muslim does not continue confused and lost in the maze of these approaches, or harbours doubts about carrying the da’wah. In what follows, we present some of the most important approaches.