4.6 Hijra (Uhamiaji) Kwenda Madina
4.6 The Hijrah (migration) To Madinah
Hata hivyo, Hijra kwenda Madina ilikuwa mpito wa da'wah kutoka hatua ya majadiliano na subira, hadi hatua ya utekelezaji baada ya kuanzishwa kwa chombo, yaani Dola ya Kiislamu. Ilikuwa ni kuhama kutoka dar al-kufr kwenda dar al-Islam, ambayo Mtume ﷺ aliianzisha Madina. Huko alikuwa ﷺ akiufikisha Uislamu kwa namna tofauti kabisa, ambayo ingefanyika kupitia Dola inayotawala kwa Uislamu, inautekeleza na kuulingania kwa dalili na hoja, na kuubeba kwa nguvu inayoilinda da'wah dhidi ya nguvu za uovu na udhalimu.
However the Hijrah to Madinah formed a transition of the da’wah from the stage of discussion and patience, to the stage of implementation after the establishment of the entity, ie the Islamic State. It is movement from dar al-kufr to dar al-Islam, which the Messenger estbalished in Madinah. There he would convey Islam in a completey different manner, which would be done through a State that rules by Islam, applies it and calls for it with evidence and proof, and carries it by the force that protects the da’wah from the forces of evil and tyranny.
Mtume ﷺ alipowasili Madinah, watu wengi wa mji huo walimpokea. Jambo la kwanza alilofanya ﷺ lilikuwa kujenga msikiti; msikiti huo ulikuwa mahali pa swala na kufanya mashauriano, na ulitumika kusimamia mambo ya watu na kusuluhisha migogoro. Alianza ﷺ kuandaa hali ya Madinah kwa vita; aliweka misafara ya kijeshi ambayo aliwateua viongozi wake na kuwatuma nje ya Madinah; alitia saini mikataba na Mayahudi. Kwa ujumla, Mtume ﷺ alipokuwa Madinah alianza kuchukua nafasi ya mtawala; kiongozi wa dola.