11.6 Demokrasia Si Shura
11.6 Democracy Is Not Shura
Mtu hajui kama acheke au alie anaposikia kauli ya mmoja wa wale watu wanaodai kuwa na elimu, anaposema kwamba Uislamu unaanza na Demokrasia na unaishia kwa udikteta.
One does not know whether to laugh or cry when one hears the statement of one of those people claiming to have knowledge, whilst saying that Islam begins with Democracy and ends with dictatorship.
Wanatoa dalili kwa kauli ya Allah : "Na shauriana nao katika mambo yao. Kisha utakapokuwa umeazimia, basi mtegemee Allah." [TMQ 3:159] Bado kipo kipengele kimoja kinachohusiana na mada yetu ambacho kinahitaji kujadiliwa, nacho ni mtazamo wao kwamba Uislamu uliridhia Demokrasia, wakati Qur'an na Sunnah zilitaja kwa kiashiria suala la Shura. Wanasema: Demokrasia si chochote zaidi ya Shura. Kama vile Demokrasia imejengwa juu ya kuchukua maoni ya watu, Uislamu pia umetuamrisha kuchukua maoni ya watu wengine. Yeye amesema: "Na shauriana nao katika mambo yao." [TMQ 3:159]; na pia amesema: "Na ambao mambo yao ni shauri baina yao." [TMQ 42:38]; na Mtume katika maisha yake ya kivitendo, ya kisiasa na ya kijeshi, alikuwa akishauriana mara kwa mara na Maswahaba wake na kuyakubali maoni yao. Kwa kuwa hii ni amri ya Qur'an na ni uhalisia wa alivyofanya Mtume ﷺ, basi Waislamu wanapaswa kuifuata. Zaidi ya hayo wanasema kwamba tofauti kati ya Shura na Demokrasia ni ya kimaneno tu. Majina tofauti si tatizo mradi maana ni zile zile.
They cite as proof the saying of Allah ; “And consult them in their affairs. Then when you have taken a decision, put your trust in Allah.” [TMQ 3:159] One idea relevant to our subject still remains to be discussed, which is their view that Islam approved of Democracy when the Qur’an and the Sunnah alluded to the subject of Shura. They say: Democracy is nothing but Shura. Just as Democracy is built on taking the opinion of people, Islam has also ordered us to take other people’s opinions. He said; “And consult them in their affairs.” [TMQ 3:159]; and He also said; “And who conduct their affairs by mutual consultation.” [TMQ 42:38]; and the Messenger in his practical, political and military life, used to constantly consult his companions and adopt their opinions. Since this is the command of the Qur’an and the reality of what the Messenger did, then Muslims should follow it. In addition they say, that the difference between Shura and Democracy is only semantic. Different names are not a problem as long as the meanings are the same.
Tunajua kwamba wale wanaoita kwenye Demokrasia ni wa aina na makundi mbalimbali. Miongoni mwao yupo mdanganyifu mwovu, na pia yupo mwenye nia njema lakini asiyejua hakika ya Demokrasia. Makundi yenye nia njema yanapaswa kujiweka mbali kabisa na mawazo kama hayo, la sivyo yatakuwa kama yule anayemwabudu Allah {SWT} kwa ujinga, na hilo litamwongoza kutenda dhambi. Ni tabia ya mtu mwenye nia njema kutubu, kujizuia na kutafakari.
We know that those who call for Democracy are of various types and groups. From amongst them you have the evil deceiver, and also the sincere one who is ignorant of the reality of Democracy. The sincere groups are required to keep far away from such ideas, otherwise they will be like the one who worships Allah out of ignorance, and it will lead him to commit sin. It is the nature of a sincere person to repent, restrain himself and reflect.
Watu kama hao waliwahi kusema kuwa Ujamaa unatokana na Uislamu, na kwamba Mtume ﷺ ndiye Imamu wao. Sasa harufu chafu ya Ujamaa imetoweka, je, watajibu vipi sasa? Vivyo hivyo kwa Demokrasia, ambayo iko katika mateso yake ya mwisho ya kifo. Basi wale wanaounga mkono wito huu wana tumaini gani? Wazo kama hili halina manufaa kwa Uislamu, bali lina manufaa kwa Demokrasia. Badala ya kufichua upotovu wake, wanalichukua kama fikra yao kuu. Wanalipeleka kwa watu badala ya kulikanyaga chini ya miguu yao.
Such people once said that Socialism is from Islam and that the Messenger is their Imaam. Now that the putrid smell of Socialism has disappeared, how will they respond now? The same applies to Democracy, which is in its final pangs of death. So what hope do the advocates of this call have? Such an idea is not for the benefit of Islam but for the benefit of Democracy. Instead of exposing its falsehood, they adopt it as their highest thought. They carry it to the people instead of crushing it under their feet.
Utekelezaji wa amri ya Allah ni kwa kufanya Neno la Allah kuwa la juu, na kufanya dini iwe ya Allah peke yake . Hili linaweza kufikiwa tu na kundi lililoongozwa katika ufahamu wake na lenye uangalifu katika kuanzishwa kwake, lililoangazwa katika itikadi yake, na lenye ufahamu wa kina wa hukumu za Shari'ah, ambalo linakataa mawazo ya kigeni na tafsiri za kigeni. Halikubali kuinama mbele ya hali halisi wala kuingia chini ya ushawishi wa mazingira.
The realisation of Allah’s command is by making the Word of Allah the highest, and making the deen exclusively for Allah . This can only be achieved by a group that is guided in its understanding and aware in its establishment, and enlightened in its creed, deep in its understanding of the Sharee’ah rules and that rejects the alien thoughts and the foreign definitions. It does not accept to bow to the reality or fall under the influence of the circumstances.