Allah ~ huingiza hofu na woga mioyoni mwa wakosefu
Allah ~ instils terror and fear in the hearts of sinners
Moyo wa mwenye dhambi daima umo katika hali ya wasiwasi na hofu, kwa sababu utii kwa Allah ~ ni ngome kubwa ya Allah, hivyo yeyote anayeingia ndani yake yuko salama kutokana na adhabu ya dunia na Akhera; lakini yeyote anayetoka humo atazungukwa na kila aina ya hofu na wasiwasi. Moyo wa mwenye dhambi daima hauna utulivu; anahisi woga kwa kila kelele anayoisikia, na anaamini kwamba msiba wowote unamlenga yeye. Lakini yule anayemcha Allah ataepushwa na wasiwasi huu wote. Dhambi huleta hisia ya kujitenga moyoni. Mwenye dhambi anajiona amejitenga na Mola wake na na watu wengine. Anapozidi kutenda dhambi, ndivyo kujitenga kwake kunavyoongezeka, na hivyo atakabiliwa na uchungu wa maisha kama mtu mwenye wasiwasi na mpweke. Mwenye dhambi hufurahi anapotenda dhambi, lakini hii ni raha ya wakati tu, kwani baadaye moyo wake hujaa wasiwasi. Siri ya jambo hili ni kwamba utii kwa Allah ~ humkaribisha mcha Mungu kwake ~, na karibu na watu anaowapenda, hata kama wako mbali naye. Kuasi amri ya Allah ~ huvutia hisia ya kuwa mbali na Allah ~, na aina kali zaidi yake ni ile ya shirki, kumshirikisha Allah.
A sinner's heart is always in state of anxiety and terror, because obedience to Allah ~ represents the great fortress of Allah, so whoever enters it is safe from the Punishment of this world and the Hereafter; but whoever leaves it would be surrounded by all aspects of fear and worry. A sinner's heart is always restless; he/she feels nervous about any noise he/she hears, and believes that any misfortune is intended for him/her. But one who fears Allah would be spared all these worries. Sins implant a sense of isolation in the heart. A sinner feels secluded from his/her Lord and from other people. As he/she commits more sins, his/her isolation increases, and so he/she would endure the bitterness of life, as a worried lonely person. A sinner feels delighted when committing a sin, but this is just a pleasure of the moment, as his/her heart is filled with anxiety afterwards. The secret in this matter is that obedience to Allah ~ brings the devout person closer to Him ~. and closer to other people that he/she loves, even if they are far away from him/her. Disobedience to Allah ~ attracts the feeling of remoteness from Allah ~. and the most severe form is that of polytheism, associating partners with Allah.