Dhambi huzuia baraka za Allah (zisifike) na huchochea ghadhabu yake.
Sins hold back the Blessings of Allah ~ (to come) and incite His Anger
Hakuna baraka inayoondolewa kutoka kwa mja wa Allah isipokuwa kwa sababu ya matendo yake mabaya mwenyewe; wala hakuna msiba wala adhabu inayomfika isipokuwa kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe. Ali bin Abi Talib alisema: "Hakuna mtihani unaoteremka isipokuwa kwa sababu ya dhambi, na haondoki isipokuwa kwa toba", kwa sababu Allah ametangaza: {Msiba wowote unaokupateni ni kwa sababu ya yale yaliyotenda mikono yenu. Naye anasamehe mengi}. Pia amesema: {Hivyo ni kwa sababu Allah habadilishi neema aliyowapa watu mpaka wao wabadilishe yaliyomo nafsini mwao}. Allah ~ anatujulisha kuwa Hatabadilisha neema alizowapa mja wake, isipokuwa mja wake akizibadilisha mwenyewe. Lakini mwenye dhambi hugeuza utii kwa Allah kuwa uasi, shukrani kwa neema za Allah kuwa kutokushukuru kwake, na sababu zinazoleta radhi za Allah kuwa sababu za laana yake. Allah ~ amesema: {Hakika Allah hatabadilisha hali ya watu mpaka wao wabadilishe hali yao wenyewe (kwa kuendelea kutenda dhambi, kutokushukuru na kutomtii Allah)}.
No blessing is removed from a Servant of Allah ~ except by his/her own misdeeds; and no misfortune or punishment befalls him/her but from his/her own sins. Ali bin Abi Talib ~ said: "No affliction comes down except due to a sin , and it is not removed except with repentance", for Allah ~ said: (Whatever of misfortune befalls you, it is because of what your hands have earned. And He pardons much Y He ~ also said: ( That is so because Allah will never change a Grace which He has bestowed on a people until they change what is in themselves. ) 2 Allah ~ informs us that He will not change the Blessings, which He ~ has bestowed upon His Servant, unless His Servant changes them for him/her self. But a sinner changes obedience to Allah into disobedience, thankfulness for the Blessings of Allah into ungratefulness towards Him ~' and the causes that lead to Allah's Pleasure into those that cause His Curse. Allah ~ said: (Verily, Allah will not change the (good) condition of a people as long as they do not change their state themselves (by continuing to commit sins and be ungrateful and disobedient to Allah)) 3
1 Surat Ash-Shura, Aya ya 30. 2 Surat Al-Anfal, Aya ya 53. 3 Surat Ar-Ra'd, Aya ya 11.
1 Surat Ash-Shura, Verse 30. 2 Surat Al-Anfal, Verse 53 . 3 Surat Ar-Ra'd, Verse 11.