Dhambi humtoa mtu nje ya wigo wa Ihsan.
Sins take a person out from the scope of lhsan
Ihsani ni ukamilifu katika kutekeleza wajibu wa mtu. Ni kumwabudu Allah kana kwamba unamuona, lakini ikiwa huwezi kumfikiria Yeye, unapaswa kukumbuka kwamba Yeye ~ anakuona. Mwenye dhambi anapoondolewa katika hali ya ihsani, huzuiwa kupata Malipo ya Allah ~' yanayotolewa kwa wale wanaofanya vizuri katika kutimiza majukumu yao ya kidini. Ihsani inapohusiana na moyo, huuzuia kutenda dhambi; kwa sababu mtu anayemwabudu Allah ~ ' kwa ukamilifu, ni yule ambaye moyo wake umejaa mapenzi, matumaini, khofu na kumkumbuka Allah ~. Anamwabudu Allah ~ kana kwamba anamwona, na hivyo anazuiwa kumwasi. Kwa hiyo, mtu anapoondolewa katika hali ya ihsani, huachwa peke yake pamoja na nafsi yake akijaribu kufurahia maisha. Allah ~ akitaka mema kwake, humweka miongoni mwa kundi la waumini; lakini akimwasi Allah ~ na kujiingiza katika madhambi, Allah ~ humwondoa katika hali ya Iman (imani njema), kama alivyosema Mtume ﷺ: "Mzinzi si mwumini wakati anapozini. Mnywaji wa pombe si mwumini wakati anaponywa pombe. Mwizi si mwumini wakati anapoiba ..." 1 Kwa hiyo, jiepushe na kutenda dhambi, za aina yoyote ile, na chukua fursa ya kutubu, wakati bado inawezekana kufanya hivyo.
lhsan is perfection in performing one's obligations. It is worshipping Allah as though you see Him, but if you are unable to imagine Him, you should remember that He ~ sees you. When a sinner is removed from the state of lhsan , he/she is deprived of receiving the Reward(s) of Allah ~' which are given to those who excel in fulfilling their religious duties. When lhsan is related to the heart, it prevents it from committing sins; because a person who worships Allah ~ ' with perfection, is one whose heart is filled with love, hope , fear and remembrance of Allah ~ - He worships Allah ~ as though he sees Him, and so he is prevented from disobeying Him. Therefore, when a person is removed from the state of lhsan , he/she is left among his/her own private company to try to enjoy life. If Allah ~ wants good for him/her, He ~ assigns him/her at the circle of the believers; but if he/she disobeys Allah ~ and indulges in sins, Allah ~ removes him/her from the state of Iman (good faith), as was said by the Prophet ~ : "A fornicator is not a believer at the time of committing fornication. The one who drinks wine is not a believer at the time of drinking wine. A thief is not a believer at the time of thieving ... " 1 Therefore, avoid committing sins , whatever their nature, and take the chance to repent, while it is still possible for you to do so .
1 Ameripokelewa na Ibn Maajah katika kitabu "Al-Fitan" (sura ya 3).
1 Recorded by lbn Maajah in the book, "Al-Fitan" (chapter 3) .