Dhambi zinaweza kumfanya mtu asahaulike na Allah ~
Sins may lead a person to become forgotten by Allah ~
Ni adhabu kwa mwenye dhambi, anayejiingiza katika madhambi, hatimaye kusahauliwa na Allah ~ na kuachwa peke yake pamoja na shetani. Hii ni hatua ya maangamizi ambayo hakuna matumaini ya usalama. Kwa maana Allah~ amesema: ( Enyi mlioamini! Mcheni Allah na mtekeleze wajibu wenu kwake. Na kila nafsi na iangalie itakalotanguliza kwa kesho, na mcheni Allah. Hakika Allah anajua yote mnayoyafanya. Wala msiwe kama wale waliomsahau Allah, naye akawafanya wajisahau nafsi zao. Hao ndio Mafasiki (waasi na wasiotii amri za Allah). ) Allah ~ ametuamuru tumche Yeye (kumkumbuka Yeye katika kila jambo letu) na ametuonya tusiige mwenendo wa wale walioasi amri Yake. Ametujulisha kuwa aliwaadhibu wale waliokataa wema, kwa kuwafanya wasahau nafsi zao, yaani wasahau manufaa yaliyoweza kuwaokoa na adhabu ya Akhera. Allah ~ aliwafanya wasahau Njia Iliyo Sawa, ambayo ingewaongoza kwenye Uzima wa Milele Peponi ambako wangefurahia neema zake kamili. Unaweza kumwona mwenye dhambi akijipotezea kwa ubinafsi manufaa ya nafsi yake, kwa kuwa moyo wake umefanywa usijali kumkumbuka Allah ~; anafuata matamanio yake mwenyewe, kwa hiyo matendo yake yamepotea, kwa sababu anakataa Malipo ya thamani ya Allah kwa mambo duni ya dunia hii! Mwenye dhambi hana wa kulaumiwa isipokuwa nafsi yake mwenyewe, kwa kuwa anaidhulumu nafsi yake, si Allah ~. Allah ~ ndiye Mtoaji wa neema zote, wala hahitaji kitu chochote kutoka kwa viumbe Vyake.
It is a punishment for a sinner, indulging in sins, to eventually be forgotten by Allah ~' and left alone with the devil. This is a stage of destruction for which there is no hope of safety. For Allah~ has said: ( 0 you who believe! Fear Allah and keep your duty to Him. And let every person look to what he has sent forth for the morrow, and fear Allah. Verily, Allah is All-Aware of what you do. And be not like those who forgot Allah, and He caused them to forget themselves. Those are the Fasiqun (rebellious and disobedient to Allah) 2 Allah ~ ordered us to fear Him (be mindful of Him in all our actions) and warned us not to imitate those who have become disobedient to Him. He ~ informed us that He puni shed those who had rejected righteousness, by letting them forget themselves - i.e. to forget the benefits which could save them from the Punishment in the Hereafter. Allah ~ made them forget the Right Path, which would lead them to the Eternal Life in Paradise where they could enjoy its perfect blessings. You may see the sinner selfishly wasting benefits for him/her self, as his heart is made heedless of remembrance Allah ~ ; he/she follows his/her own lusts, so his/her deeds have been lost, because he/she rejects the priceless Reward of Allah for the meagre affairs of this world! A sinner only has him/her self to blame, for he/she is unjust to him/her self, not to Allah ~ - Allah ~ is the Provider of all Blessings, and is not in need of anything from His Creatures.