Aina za mapenzi
Types of love
Kuna aina nne za mapenzi, ambazo ni lazima zitofautishwe baina yake, na yeyote asiyeweza kuzitofautisha hakika amepotea njia. Ya kwanza, mapenzi kwa Allah; haya peke yake hayatoshi kumwokoa mtu na Adhabu ya Allah, wala kupata Malipo Yake, kwani washirikina, wanaoabudu Msalaba (Wakristo), na Mayahudi wanadai kumpenda Allah. Ya pili, kupenda anachokipenda Allah. Ni aina hii ambayo humwingiza mtu katika Uislamu na kumtoa katika ushirikina. Watu wapendwa zaidi kwa Allah ni wale wanaolitunza vizuri aina hii ya mapenzi. Ya tatu, kupenda kwa ajili ya Allah, ambayo ni moja ya masharti ya kupenda anachokipenda Yeye. Ya nne, kuelekeza mapenzi ya mtu kwa wengine badala ya Allah; kumpenda Allah na sanamu nyinginezo kwa wakati mmoja. Hii ni mapenzi ya washirikina. Yeyote anayewapenda wengine pamoja na Allah, si kwa ajili ya Allah, basi amewachukua kuwa miungu mingine badala ya Allah. Kuna aina nyingine ya tano ya mapenzi, ambayo haimo katika mada yetu. Ni mapenzi ya asili ya mwanadamu kwa vitu vinavyofaa maumbile yake; kama vile mapenzi ya mwenye kiu kwa maji, na mwenye njaa kwa chakula; mapenzi ya usingizi, mke na watoto. Hizi ni aina za mapenzi ambazo hazikosolewi, isipokuwa zinapomvuruga mtu kutoka kumkumbuka Allah na kumpenda Yeye. Allah ametuambia: {Enyi mlioamini! Mali zenu wala watoto wenu wasikuvuruge kutoka katika kumkumbuka Allah}, na pia Amesema: {Watu ambao biashara wala kuuza hakuwavurugi kutoka katika kumkumbuka Allah.}2