Dhulma na Ukandamizaji
Tyranny and Oppression
Dhulma na udhalimu ni miongoni mwa dhambi kubwa kabisa kwa sababu zinapingana na haki, ambayo mbingu na ardhi zilisimamishwa juu yake. Allah ~ aliwatuma Mitume Wake na Vitabu Vyake ili watu wapate kusimamisha haki miongoni mwao. Kuua bila haki, bila sababu yoyote ya kisheria, ni dhambi kubwa. Uislamu unataja mifano mingi ya vitendo viovu kama hivyo, kama vile kumuua mtoto wa mtu kwa kuogopa kwamba mtoto huyo atashiriki riziki yake (yaani chakula, kinywaji na mali); kumuua wazazi wa mtu ambao ndio sababu ya kuwepo kwake; na kuwaua jamaa wa karibu. Ukubwa wa kitendo hicho kiovu hutofautiana kulingana na asili ya kitendo chenyewe. Kwa hiyo, mtu atakayepata adhabu kali kabisa Siku ya Kiyama ni yule aliyemuua nabii, kisha yule aliyemuua Imamu, au mwanachuoni aliyeamrisha haki miongoni mwa watu na kuwalingania kwenye Njia ya Allah ~. Allah ~ ameweka adhabu ya kuua kwa makusudi muumini kuwa ni kudumu milele Motoni, pamoja na Laana na Ghadhabu ya Mola.
Tyranny and oppression are among the greatest sins because they oppose justice, upon which the heavens and the earth were established. Allah ~ sent His Messengers and Books in order that people might establish justice among themselves. The act of killing unlawfully, without any right, is a great sin. Islam cites many examples of such evil acts, like the killing of one's child for fear that the child might share one's provision (i.e. food, drink, and money); the killing of one's parents who were the cause of one's existence; the killing of one's kin. The grade of such an evil act differs according to the nature of the act itself; therefore, the person who will receive the utmost punishment on the Day of Resurrection is the one who killed a prophet, followed by the one who killed an Imam, or a scholar who commanded justice among people and invited them to the Path of Allah ~- Allah ~ has set the punishment for the intentional killing of a believer as dwelling eternally in the Hell-Fire, with the Curse and Anger of the Lord.