13.3 Uchaguzi wa wajumbe wa baraza la Ummah
13.3 The election of the members of the Ummah’s council
KUCHAGUA WAJUMBE WA BARAZA LA UMMAH
ELECTING THE MEMBERS OF THE COUNCIL OF THE UMMAH
Wajumbe wa Baraza la Ummah wanachaguliwa, si kuteuliwa. Wao ni wawakilishi wa watu katika kutoa maoni, na mwakilishi ni lazima achaguliwe na yule anayemwakilisha, wala asilazimishwe kwake kamwe. Pia, kwa kuwa wajumbe wa Baraza la Ummah ni wawakilishi wa maoni ya watu, iwe ni watu binafsi au makundi, basi kujua mwakilishi wa watu katika eneo kubwa na kwa wananchi wasiohesabika hakuwezekani isipokuwa mwakilishi huyu achaguliwe nao.
The members of the Ummah's Council are elected and not appointed. They are representatives of the people in the voicing of opinions, and the representative should be chosen by the person whom he represents and should never be imposed upon him. Since also the members of the Ummah's Council are representatives of the people's opinions, whether they are individuals or groups; so to know the representative of people in a large area and the uncounted folk does not come about unless this representative is chosen by them. .
Zaidi ya hayo, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (SAW) hakuwachagua wale aliowashauri kwa msingi wa uwezo wao, umahiri wao na haiba zao; badala yake aliwachagua kwa misingi miwili: Kwanza, kwa sababu walikuwa viongozi miongoni mwa kaumu zao, bila kujali uwezo na umahiri wao; pili, kwa sababu waliwakilisha Muhajirina na Answari. Sababu ya kuwepo kwa watu wa Shura ni kuwakilisha watu. Kwa hiyo kanuni ambayo wajumbe wa Baraza la Ummah wanapaswa kuchaguliwa nayo ni: uwakilishi wa watu, kama ilivyokuwa katika uteuzi wa makusudi kutoka miongoni mwa viongozi, na uwakilishi wa makundi, kama ilivyokuwa katika uteuzi wa makusudi kutoka miongoni mwa Muhajirina na Answari. Uwakilishi huu wa watu binafsi na makundi ambayo hayahesabiki hauwezi kupatikana isipokuwa kwa uchaguzi. Wajumbe wa Baraza la Ummah hivyo ni lazima wachaguliwe kwa kura.
Moreover, the Messenger of Allah (PBUH) did not choose those whom he consulted based on their ability, competence and personalities; rather he chose them based on two points: Firstly, because they were chiefs among their folks, regardless of their ability and competence; secondly, because they represented the Muhajireen and the Ansar. The reason for the presence of the people of the Shura is to represent the people. Therefore the tenet upon which the Ummah's Council members are chosen should be: the representation of people, as was the case in the deliberate selection from the chiefs, and the representation of the groups as was the case in the deliberate selection from the Muhajireen and the Ansar. This representation of the individuals and groups who are uncounted cannot be achieved except by election. The members of the Ummah's Council have to therefore be elected. .
Kuhusu kwamba ni Mjumbe wa Allah ﷺ mwenyewe aliyechagua ni nani alimshauriana naye, hii ilitokana na ukweli kwamba eneo husika, Madina, lilikuwa dogo, na kwamba Waislamu walikuwa wanajulikana kwake. Kwa upande mwingine, katika Bay'ah ya pili ya Al-Aqaba, Waislamu waliompa Bay'ah hawakuwa wanajulikana kwake, na ndiyo sababu aliuacha suala la kuchagua viongozi kwao, akisema: .
As for the fact that it was the Messenger of Allah (PBUH), himself, who chose whom he consulted, this was because the area in question, Medina, was small and because the Muslims were known to him. In contrast, in the second Bayah of Al-Aqaba, the Muslims who gave him the Bayah were not known to him and this is why he left the matter of choosing the chiefs to them, by saying: .
"Mchagueni miongoni mwenu viongozi kumi na wawili ambao watawajibika kwa nafsi zao na kwa watu wao." Imepokewa katika Sira ya Ibn Hisham kutoka kwa Ka'b bin Malik. Kwa hivyo tunaweza kuhitimisha kutokana na ukweli kwamba wajumbe wa Baraza la Ummah wanawakilisha maoni ya Waislamu kwa ujumla. Na kwa kuwa sababu ('Illah) ya kuanzishwa kwa Baraza ni kuwawakilisha watu binafsi na makundi katika kutoa maoni yao na kuwawajibisha watawala, na kwa kuwa hili haliwezi kutimizwa ikiwa watu hao hawakujulikana, isipokuwa kukiwa na uchaguzi wa jumla. Yote haya yanathibitisha kwamba wajumbe wa Baraza la Ummah wanapaswa kuchaguliwa, na si kuteuliwa.
"Choose from among you twelve leaders who will be responsible for themselves and their people." As reported in the Seerah of Ibn Hisham from Kaab b. Malik. We can thus conclude from the fact that the members of the Ummah's Council represent the opinion of the Muslims at large, and since the reason (‘Illah) for which the Council is founded is to represent the individuals and groups in voicing their opinions and in holding the rulers accountable, and since this cannot be achieved if the persons were not known, unless there was a general election. All of this proves that the members of the Ummah's Council should be elected and not appointed.