4.4 Njia ya kumteua Khalifa
4.4 The method of appointing the Khalifa
Wakati Shara ilipofanya iwe wajibu kwa Ummah kumteua Khalifah, ilibainisha kwa ajili yake njia ambayo Khalifah anateuliwa. Njia hii imethibitishwa katika Kitabu na Sunnah. Waislamu ambao lazima watoe bay'ah ni wale ambao ni raia wa Khilafah wakati huo. Katika hali ambayo hakuna Khilafah, Waislamu wanaohusika kutoa bay'ah ni wale wanaoishi katika eneo ambalo Khilafah inapaswa kutekelezwa.
When Shara made it incumbent upon the Ummah to appoint a Khalifah, it determined for her the method by which the Khalifah is appointed. This method is proven in the Book and the Sunnah. The Muslims who must give the bayah are those that are citizens of the Khilafah at that time. In the case where there is no Khilafah the Muslims responsible for giving the bayah are those living in the region where the Khilafah should be implemented. .
Njia ya kumchagua Khalifah kwa bay'ah imethibitishwa kutokana na mfano wa Bay'ah ambayo Waislamu walimpa Mtume (S.A.W.), na kutokana na amri ya Mtume ﷺ kwetu, ya kumpa Imamu Bay'ah. Bay'ah ya Waislamu kwa Mtume ﷺ haikuwa Bay'ah juu ya Utume, bali ilikuwa Bay'ah juu ya utawala, kwa kuwa ilihusu kitendo si imani. Kwa hiyo, Rasuli wa Allah ﷺ alipewa kiapo cha utii kama mtawala, wala si kama Nabii au Mtume ﷺ. Hii ni kwa sababu kukubali Unabii na Utume kunahusishwa na imani (Iman), wala si Bay'ah. Hivyo, Bay'ah kwake ﷺ ilikuwa tu kwa nafasi yake kama kiongozi wa dola.