9.2 Masharti ya mahakimu
9.2 The conditions of the judges
Yeyote anayechukua wadhifa wa kuwa qadhi lazima awe Mwislamu, mtu huru, aliyebaleghe, mwenye akili timamu, mwadilifu, Faqih (mwanachuoni mwenye elimu ya fiqhi), na mwenye ujuzi wa jinsi ya kutumia hukumu za Kiislamu kwenye uhalisia (li-tanzil al-ahkam ‘ala ’l-waqi’). Kuhusu mtu anayechukua ukadhi wa Mazalim, mbali na masharti yaliyotajwa, lazima pia awe mwanaume na Mujtahid (mwanachuoni wa ijtihadi), kama ilivyo kwa Qadi al-Qudah (Qadhi Mkuu), kwa sababu wadhifa huu kwa hakika ni ukadhi na utawala, kwani anahukumu juu ya mtawala na kutekeleza Shariah juu yake. Kwa hiyo lazima awe mwanaume pamoja na masharti mengine ya wadhifa wa qadhi; mojawapo likiwa ni kuwa Faqih. Zaidi ya hayo, ni lazima awe Mujtahid, kwa sababu sehemu ya Mazalim ambayo anaweza kuhitajika kuichunguza ni iwapo mtawala ametawala kwa kile kisicho alichokiteremsha Allah, yaani, ametawala kwa sheria isiyo na dalili ya Shariah inayoiunga mkono, au endapo dalili aliyoitumia haihusiani na tukio husika, na ni Mujtahid pekee awezaye kushughulikia Madhlima ya namna hiyo. Kwa hiyo, asipokuwa Mujtahid, atakuwa anahukumu bila kuwa na elimu; na hilo ni haramu. Basi, mbali na masharti ya mtawala na yale ya qadhi, pia anapaswa kuwa Mujtahid.
Anyone taking up the post of judge must be a Muslim, free, mature, sane, just, a Faqih (learned scholar), and aware of how to apply the Islamic rulings to the reality (li-tanzil al-ahkam ‘ala ’l-waqi’). As for the person who takes up the judiciary of Mazalim, in addition to the conditions mentioned, he must also be male and a Mujtahid (legist), just like the supreme judge (Qadi al-Qudah), because this post is in fact judiciary and ruling, for he judges over the ruler and executes the Shariah upon him. Therefore he must be male in addition to the other conditions of the post of judge; one of which is to be a Faqih. Furthermore, he has to be a Mujtahid, because part of the Mazalim which he may be required to look into is whether the ruler has ruled by other than that which Allah has revealed, i.e. ruled by a law that has no Shariah evidence to back it, or in case the evidence he used does not relate to the event, and only the Mujtahid can deal with such Madhlima. Therefore if he were not a Mujtahid, he would be judging without having knowledge; and that is forbidden. Therefore, in addition to the conditions of the ruler and those of the judge, he should also be a Mujtahid.