13 Baraza la Umma
13 The Council of the Ummah
Hili ni Baraza lililoundwa na watu wanaowakilisha maoni ya Waislamu kwa ujumla, ambao Khalifah anaweza kuwarejea kuwashauri katika masuala mbalimbali. Nao, kwa upande wao, ni wawakilishi wa Ummah katika kuwawajibisha watawala. Hili linatokana na uteuzi wa Mjumbe wa Allah ﷺ wa wakuu kumi na wane (Nuqaba') kutoka miongoni mwa Ansar na Muhajireen ili wafanye mashauriano nao kuhusu mambo. Pia linatokana na ukweli kwamba Abu Bakr (rta) aliwateua baadhi ya watu kutoka miongoni mwa Muhajireen na Ansar awarejee kwa ajili ya kutaka maoni yao pale jambo lilipotokea. Watu wa Shura wakati wa Abu Bakr (rta) walikuwa ni Ulama na watu wa Fatwa. Ibn Sa'd ameripoti kutoka kwa Al-Qasim kwamba pale jambo lilipotokea na Abu Bakr alitaka kushauriana na watu wa maoni na watu wa Fiqh, aliwaita kutoka miongoni mwa Muhajireen na Ansar: 'Umar, 'Uthman, Ali, Abdur Rahman bin Awf, Mu'adh bin Jabal, Ubayy bin Ka'b na Zayd bin Thabit. Wote hao walikuwa wakitoa maoni yao wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr. Watu pia walikuwa wakichukua Fatwa zao. 'Umar alipokuwa Khalifah naye alikuwa akiwaita watu hawa, ilhali Fatwa wakati wa utawala wake zilitolewa kwa 'Uthman, Ubayy na Zayd. Hili linaonyesha kwamba inaruhusiwa kuanzisha Baraza maalum linalowakilisha Ummah katika kuwawajibisha watawala, na kushiriki katika Shura. Hili linathibitishwa na nasi kutoka Qur'an na Sunnah. Linaitwa Baraza la Ummah kwa sababu linawakilisha Ummah katika uwajibikaji na mashauriano.
This is a Council formed of individuals representing the opinion of the Muslims at large, to whom the Khaleefah can refer to consult them on various issues. They in turn are the representatives of the Ummah in holding the rulers accountable. This is deduced from the Messenger of Allah’s (pbuh) nomination of fourteen chiefs (Nuqaba’) from the Ansar and the Muhajireen in order to consult with them about matters. It is also deduced from the fact that Abu Bakr (rta) designated some men from the Muhajireen and the Ansar to refer to them seeking their opinion when something happened. The people of the Shura at the time of Abu Bakr (rta) were the Ulama and the people of Fatwa. Ibnu Sa’d reported from Al-Qasim that when something happened and Abu Bakr wanted to consult the people of opinion and the people of Fiqh, He called from the Muhajireen and the Ansar; ‘Umar, ‘Uthman, Ali, Abdur Rahman bin Awf, Mu’az bin Jabal, Ubai bin Ka’ab and Zaid bin Thabit. They all used to give their opinion during the Khilafah of Abu Bakr. People would also take their Fatwa. When ‘Umar became Khaleefah He would also call these people, while the Fatwa in his time was to ‘Uthman, ‘Ubai and Zaid. This indicates that it is permitted to set up a special Council that represents the Ummah in holding the rulers accountable, and to participate in the Shura. This is confirmed by texts from the Qur’an and the Sunnah. It is called the Council of the Ummah because it represents the Ummah in accounting and consultation.
Inaruhusiwa kwa raia wasio Waislamu kuwa wanachama wa Baraza, ili waweze kuwasilisha malalamiko dhidi ya dhuluma yoyote inayofanywa dhidi yao na watawala, au dhidi ya utekelezaji usio sahihi wa Uislamu juu yao.
It is permitted for non-Muslim citizens to be members of the Council, in order to file complaints against any injustice perpetrated against them by the rulers or against any mis-implementation of Islam upon them.