15 Uislamu unakataza kutawala kwa dola la polisi
15 Islam forbids ruling by a police state
Utawala na mamlaka katika Uislamu maana yake ni kusimamia mambo ya watu kwa kutumia hukumu za Shari'ah. Hii si sawa na kufanya hivyo kwa nguvu, kwani nguvu ndani ya Dola haikusudiwi kuwalinda watu au kusimamia mambo yao. Nguvu si mamlaka, ingawa kuwepo kwake, kuundwa kwake, kuendeshwa kwake na kuandaliwa kwake hakutokei bila mamlaka. Nguvu ni kitu cha kimwili kinachojidhihirisha katika umbo la vikosi vya kijeshi, pamoja na jeshi la polisi, ambavyo mamlaka hutumia kutekeleza hukumu, kuwashinda wahalifu na waasi, kuwakandamiza wanaoasi sheria, kuzuia wachokozi, na kuvitumia kama chombo cha kulinda mamlaka yenyewe na mawazo na fikra zinazoyasimamia, na kuyafikisha kwa ulimwengu.
Ruling and authority in Islam mean running the affairs of the people by applying the Shari’ah rules. This is not the same as doing this by force, for force within the State is not designed to look after people, or to manage their affairs. Force is not the authority, although its existence, formation, administration and preparation do not come about without authority. Force is a physical entity that manifests itself in the shape of the armed forces-including the police force-with which the authority executes the rules, defeats the criminals and the rebels, oppresses the outlaws, curbs the aggressors and uses it as a tool to protect the authority and the concepts and thoughts on which it is founded and to convey them to the world.