14 Uislamu lazima utekelezwe kwa ujumla. Utekelezaji wa taratibu ni Haramu.
14 Islam must be implemented as a whole. Gradual implementation is Haram
Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ kwa sehemu sehemu kulingana na matukio na mambo yaliyojiri, na kila mara aya moja ilipoteremshwa, yeye ﷺ alikuwa akiifikisha mara moja. Ikiwa aya ilikuwa na amri, yeye ﷺ pamoja na Waislamu walikuwa wakiitekeleza mara moja, na ikiwa aya ilikuwa na katazo, yeye ﷺ pamoja na Waislamu walikuwa wakajizuia na kuacha kufanya jambo hilo mara moja. Utekelezaji wa hukumu ulikuwa ukianza mara baada ya kuteremshwa, bila kuchelewa. Hukumu yoyote iliyoteremshwa ilikuwa ikiwa wajibu wa kutekelezwa na kufanyiwa kazi mara ilipoteremshwa, chochote hukumu hiyo ilivyokuwa, hadi Mwenyezi Mungu (SWT) alipoikamilisha Dini hii na akateremsha kauli yake (SWT): "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu." [TMQ Al-Ma’idah: 3]
The Holy Qur’an was revealed to the Messenger of Allah (pbuh) in parts according to the events and incidents, and each time a verse was revealed, He (pbuh) would convey it at once. If the verse contained a command, He (pbuh) and the Muslims would execute it at once and if the verse contained a prohibition, He (pbuh) and the Muslims would at once refrain and abstain from doing it. The implementation of the rules used to take immediate effect after their revelation, without any delay. The rule that was revealed would become due for implementation and execution the moment it is revealed, whatever the rule was, until Allah (swt) completed this Deen and revealed His (swt) saying; “Today I have completed your Deen for you completed My favour upon you and have chosen for you Islam as your Deen.” [TMQ Al-Ma’idah: 3]