4.19 Kuondolewa kwa Khalifa
4.19 The removal of the Khaleefah
Khalifa huondolewa mara moja iwapo hali yake itabadilika kwa namna inayomtoa katika wadhifa wa Ukhalifa. Khalifa lazima aondolewe iwapo hali yake itabadilika kwa namna isiyomtoa katika wadhifa wa Ukhalifa, lakini Shariá haimruhusu kuendelea katika wadhifa wake.
The Khaleefah is removed immediately if his status changed in a way that takes him out from the post of the Khilafah. The Khaleefah must be removed if his status changes in a way that does not take him out from the post of the Khilafah, but He is not allowed by Shar’a to continue in his post.
Tofauti kati ya hali inayomtoa Khalifah katika cheo cha Ukhalifa na hali ambayo lazima aondolewe ni kwamba katika hali ya kwanza, utiifu hauwi wa lazima mara tu hadhi yake inapobadilika. Ilhali katika hali ya pili, ambayo lazima aondolewe, utiifu wake unabaki wa lazima hadi pale atakapoondolewa kwa vitendo.
The difference between the case that takes the Khaleefah out from the post of the Khilafah, and the case in which He must be removed is that in the first case, obedience is not compulsory as soon as his status changes. While in the second case, where He must be removed, his obedience remains compulsory until He is effectively removed.