19 Hifadhi (Hima) kwa Maslahi ya Umma
19 Seclusion (Hima) in the Public Interests
Kuna haki kwa watu wote ya kunufaika na huduma za umma, kwa madhumuni ambayo yamewekwa kwayo. Haziwezi kutumiwa isipokuwa kwa madhumuni ambayo zimewekwa kwayo. Hivyo, haijuzu kutumia barabara kwa ajili ya mapumziko (kuegesha kwa ajili ya kupumzika), wala kuegesha kwa ajili ya biashara, wala chochote ambacho barabara haikuwepo kwa ajili yake. Hii ni kwa sababu barabara imekuwepo kwa ajili ya kupitia juu yake; isipokuwa iwe inatumiwa kwa namna ambayo haizuii kupita, na matumizi haya ya pembeni yanakadiriwa kuwa ni yale yasiyosababisha madhara wala ugumu kwa wapita njia. Mito nayo haipaswi kutumiwa kwa jambo lisilo lile ambalo imekuwepo kwa ajili yake. Hivyo, ikiwa mto upo kwa ajili ya umwagiliaji, kama ilivyo kwa mfano mto mdogo, basi usitumiwe kwa usafirishaji wa majini (kusafirisha meli), ilhali ikiwa upo kwa ajili ya mambo yote mawili, kama vile Mto Nile na Mto Tigris, unaweza kutumiwa kwa yote mawili.
There is a right for all the people to benefit from the public utilities, for the purpose for which they are designated. They should not be used except for the purpose for which they are designated. Thus, it is not allowed to use a road for the purpose of a recess (parking for a break), nor parking to trade, nor anything that the road did not exist for. This is because the road exists for the purpose of travelling upon it; unless it were to be used in such a way that does not interfere with travelling; and this marginal use is evaluated as that which does not cause harm or difficulty for passers by. Rivers also should not be used for other than the matter, which they exist for. So if a river exists for irrigation, as would be the case for example with a small river, then it should not be used for navigation (shipping), while if it exists for both matters, like the Nile and Tigris, it may be used for both.