21 Bait ul Mal (Hazina ya Serikali)
21 Bait ul Mal (The State Treasury)
Bait ul-Mal ni mamlaka inayohusika na kila mapato (revenue) au matumizi, ambayo Waislamu wana haki nayo. Kwa hiyo, kila mali (Mal) ambayo Waislamu wana haki nayo, na ambayo mmiliki wake hajabainishwa, hupewa Bait ul-Mal, hata kama mmiliki wake kama kundi alikuwa amebainishwa. Mara mali inapopokelewa, basi kwa kupokelewa kwake huongezwa kwenye haki za Bait ul-Mal, iwe mali hiyo imeingia kweli katika milki yake au la, kwa sababu Bait ul-Mal ni mamlaka na si mahali tu. Na kila haki ambayo inastahili kutumika kwa maslahi ya Waislamu ni haki juu ya Bait ul-Mal. Ikiwa imetumika katika eneo lake lililobainishwa, basi huongezwa kwenye matumizi ya Bait ul-Mal, iwe imetoka mikononi mwake au la. Kwa kuwa kile kilichowafikia watawala wa Waislamu, au kinachotumiwa nao, basi sheria ya Bait ul-Mal inakitumikia, iwe kama mapato au matumizi.
The Bait ul-Mal is the authority responsible for every income (revenue) or expense, which the Muslims are entitled to. Therefore, every property (Mal) that the Muslims are entitled to, and whose owner is not assigned, is assigned to the Bait ul-Mal, even if its owner as a category was assigned. Once the property was received, then by its receipt it is added to the rights of the Bait ul-Mal, whether the property actually entered into its possession or not, because the Bait ul- Mal is an authority and not just a place. And every right, which is due to be spent on the Muslims interests, is a right upon the Bait ul-Mal. If it was spent in its specified area then it becomes added to the expenses of the Bait ul-Mal, whether it left its hold or not. Because that which reached the governors of Muslims, or is spent by them, then the law of the Bait ul- Mal applies to it, whether as revenue or expenses.