22 Kugawanya Mali miongoni mwa Watu
22 Distributing Wealth among the People
Uislamu unaruhusu umiliki wa mtu binafsi, lakini umeweka namna ya umiliki huo. Umemruhusu mtu kutumia kwa uhuru kile anachomiliki, lakini pia umeweka namna ya kukitumia. Uislamu umezingatia tofauti zilizopo kati ya binadamu katika uwezo wa kimwili na kiakili; kwa hiyo umeweka utaratibu wa kuwasaidia wanyonge na wahitaji, kwa kuwaamuru matajiri kuwapa maskini na wahitaji. Uislamu pia umezifanya huduma muhimu ambazo kwa asili yake ni za lazima kwa jamii kuwa mali ya umma kwa Waislamu wote, na umekataza mtu yeyote kumiliki kibinafsi au kujihifadhia mwenyewe au kwa wengine huduma kama hizo. Umeikabidhi pia Dola jukumu la kutoa utajiri, iwe kwa bidhaa au kwa huduma, na umeiruhusu Dola kumiliki peke yake baadhi ya mali.
Islam allows individual ownership, but has determined the manner of ownership. It has permitted the individual to freely dispose of what He or she owns, but it has also determined the manner of disposal. Islam has taken into account the disparity in the physical and mental abilities among the humans; therefore it has made provision to help the weak and the needy, by commanding the wealthy to give to the poor and needy. Islam has also made the utilities, which are in their nature indispensable to the community, a public property for all Muslims, and has forbidden any person from privately owning or protecting for himself or for others such utilities. It has also delegated the responsibility of providing the wealth, either as commodities or as services, to the State, and it has also permitted the State to exclusively acquire certain properties.