1. Utangulizi
1.Introduction
Utangulizi
Preface
Ummah ya Kiislamu imeishi bila Khilafah (Dola ya Kiislamu) kwa zaidi ya miongo saba, ikiteseka kwa upande mmoja kutokana na utawala wa mataifa ya Magharibi ya kikoloni, na kwa upande mwingine ikiathiriwa na kuingia kwa mawazo geni kwa Uislamu - kama vile usekula, utaifa na ubinafsi - katika akili za Ummah.
The Muslim Ummah have been living without the Khilafah (Islamic State) for over seven decades, plagued on the one hand by the domination of the colonialist Western nations, and on the other hand, afflicted by the infiltration of ideas alien to Islam - such as secularism, nationalism and individualism - into the minds of the Ummah.
Mahali pa Mifumo ya Kiislamu, iliyotekelezwa chini ya bendera ya Dola moja ya Khilafah kwa zaidi ya miaka 1300, ikitoa haki na usalama kwa wote waliokuwa chini yake, dunia kwa mara nyingine imetawaliwa na ufisadi, umaskini na machafuko. Kwa hakika, haya ndiyo matokeo ya asili ya njia yoyote ya maisha inayojengwa juu ya misingi dhaifu ya sheria zilizotungwa na binadamu.