Mwanaume anaweza kuchukua nafasi mbalimbali kuhusiana na uhusiano wake na watu walio karibu naye. Uislamu unabainisha haki na wajibu tofauti kwa mwanaume kulingana na nafasi anayotenda. Baadhi ya nafasi anazoweza kuwa nazo ni kama:
A man can take different roles with regard to his relationship with those around him. Islam defines different rights and duties for the man depending on which capacity he is acting in. Some of the roles he could have are as :
Mjomba wa upande wa mama / Mjomba wa upande wa baba
Maternal/ Paternal Uncle.
Mpwa wa Mama / Mpwa wa Baba.
Maternal / Paternal Nephew.
Mwanaume asiyehusiana.
Unrelated man.
Baadhi ya mifano ya haki na wajibu mbalimbali unaoangukia mwanamume kulingana na uwezo wake ni:
Some examples of the different rights and duties incumbent upon the man depending on his capacity are :
Baba ana wajibu wa kuwapa watoto wake chakula, makazi na mavazi, mpaka wakati watakapofikia umri wa kubalehe na kuweza kujitegemea. Baada ya hapo, msaada wake unakuwa sadaka.
The father must provide food, shelter and clothing for his children, until such a time that they are mature, and able to support themselves, after which his support becomes a charity.
‘A’isha (ra) amesimulia kwamba Hind binti Utbah alimwendea Mjumbe wa Allah ﷺ, akasema, “Ee Rasulullah, Abu Sufyan ni mtu bakhili, na sina chochote kutoka kwake isipokuwa kile ninachojichukulia mwenyewe.” Nabii ﷺ akasema, “Chukua kinachokutosha wewe na mtoto wako kwa haki.” Kitab al Umm, Imam Shafi‘i.
‘A’isha (ra) narrated that Hind bint Utbah came to the Messenger of Allah (saw) and she said, “Oh Rasul Allah, Abu Sufyan is a miserly man and I have nothing from him except what I take for myself.” The Prophet (saw) said, “Take what is sufficient for you and your child with justice.” Kitab al Umm, Imam Shafi‘i.
Mtoto analazimika (yaani ni fardhi) kuwatii mama au baba katika mambo yanayoruhusiwa (mubah) na ambayo ni haki ya mzazi, kwa mfano kuwahudumia au kuwatunza; na inapendekezwa (mandub) kuwatii katika mambo ambayo ni chaguo la mtoto, kwa mfano ni nani wa kuoa, na nini cha kuvaa n.k. Ni haramu kwake kuwatii wazazi wake iwapo wataamuru kumwasi Allah (SWT).
The son is obliged (i.e. it is fard) to obey the mother or father in those areas which are mubah (permitted) and are the right of the parent, e.g. to serve them or look after them, and is mandub (recommended) to obey them in areas which are the choice of the son, e.g. who to marry, what to wear etc. It is forbidden for him to obey his parents if they order him to disobey Allah (swt).
“Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake. Mama yake alimbeba kwa taabu juu ya taabu, na kumnyonyesha kwake kulikuwa ndani ya miaka miwili: (Sikilizeni amri hii) Nishukuruni Mimi na wazazi wenu; marejeo yenu ni kwangu. Lakini wakikutaka umshirikishe Mimi na kitu ambacho huna ujuzi nacho, usiwatii.” [TMQ 31:14-15].
“And we have enjoined upon man to be good to his parents. In travail upon travail did his mother bear him. And in years twain was his weaning : (Hear the command) Show gratitude to Me and your parents : To me is (your final) goal. But if they strive to make you join in worship with me things of that which you have no knowledge, obey them not.” [TMQ 31:14-15].
Ni haramu kwa mwanamume asiye mahusiano ya kifamilia na mwanamke kumtazama kwa nia ya tamaa.
It is forbidden for an unrelated man to gaze at a woman with lustful intentions.
Jarir bin ‘Abdullah alisimulia, “Nilimuuliza Mjumbe wa Allah ﷺ kuhusu kutazama kwa ghafla (kunakotokea) usoni (mwa mtu asiye mahram). Aliniamuru nigeuze macho yangu.” Muslim.
Jarir ibn ‘Abdullah reported, “I asked Allah’s Messenger about the sudden glance (that is cast) on the face (of a non-mahram). He commanded me that I should turn away my eyes.” Muslim.