Tofauti pekee kati ya watu mbele ya Allah (swt) ni kwa kiwango cha ufahamu wao wa Allah (swt) na uchamungu wao. Binadamu wote wanahitaji mfumo wa kuendesha maisha yao unaohakikisha haki na kuleta maelewano kati ya wanachama tofauti wa jamii. Mfumo huo hauwezi kamwe kuwa mfumo wa kibinadamu, kwani mwanadamu ana uwezo mdogo, ni dhaifu, mhitaji, na hana uelewa kamili wa maisha na ulimwengu. Mipango ya binadamu daima itaathiriwa na matamanio na matakwa yake, na haiwezi kamwe kufikia haki ya kweli. Katika historia yote, hata tukiangalia tamaduni na ustaarabu mbalimbali uliokuwepo na kuendesha mambo yake kwa sheria na kanuni za kibinadamu, bila shaka tunakuta dhuluma na ukosefu wa haki katika nchi. Mifano ni pamoja na ustaarabu wa kale wa Misri ambapo Mafarao walichukuliwa kuwa miungu, au Dola ya Kirumi, ambapo Kaisari alipewa sifa za uungu. Katika kesi zote mbili viongozi ndio walikuwa na neno la mwisho kuhusu sheria zipi zitawatawala watu. Matokeo yake yalikuwa ukosefu wa haki, udhalimu na ubaguzi kati ya matabaka na jamii mbalimbali za watu. Hata katika zama hizi, dhana kama ‘kabila dogo’ (ethnic minority) na ‘taifa-dola’ (nation state) zinawatambua watu kuwa wenye hadhi tofauti kwa asili yao, na hizi ni chanzo kikubwa cha ubaguzi. Lakini mafundisho ya Kiislamu, yalipotekelezwa, ndiyo mafundisho pekee yaliyofanikiwa kuwaunganisha watu pamoja bila kujali rangi zao, asili yao au utaifa wao. Allah (swt) anawalazimisha watu wote kutawala kwa mujibu wa sheria Zake. Anasema katika Qur’an: “Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoteremsha Allah, basi hao ndio makafiri.” [TMQ 5:44] Mafundisho haya yanafanya kazi kwa sababu yanawachukulia watu kama binadamu tu, na kwa sababu vyanzo vyake vya sheria havitoki kwa mwanadamu. Allah (swt) anasema: “Na katika ishara Zake ni kuumbwa mbingu na ardhi, na tofauti ya lugha zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo mna ishara kwa wenye kujua.” [TMQ 30,22] UONGO: Katika Uislamu wanawake hawapewi haki sawa na wanaume. Wanachukuliwa kuwa daraja la pili, wananyanyaswa, na wanazuiwa kuwa na sauti katika mambo yao binafsi na mambo ya umma.
The only difference between people as far as Allah (swt) is concerned is with regard to their awareness of Allah (swt) and their piety. All human beings need a system to run their lives that ensures justice and establishes harmony between the different members of the society. That system can never be a man-made system, since man is limited in his capability, weak, needy and lacks a comprehensive understanding of life and the universe. Man’s designs will always be subject to whims and desires and can never achieve true justice. Throughout history, even if we look at the different cultures and civilisations that existed and ran their affairs by man-made laws and regulations, we definitely find oppression and injustice in the land. Examples include the ancient Egyptian civilisations where the Pharaohs were seen as gods, or the Roman Empire, where the Caesar was ascribed the attributes of divinity. In both these cases the leaders had the final say in what laws should govern the people. The result was injustice, tyranny and discrimination between different classes and races of people. Even in the modern day, concepts such as ‘ethnic minority’ and ‘nation state’ recognise people to be of inherently different status - these are a source of much discrimination. The Islamic doctrine, however, when it was implemented, was the only doctrine that managed to unite people together without any consideration of their race, colour or nationality. Allah (swt) obliges all people to rule according to His laws. He (swt) states in the Qur’an, “Whoever does not rule by whatever Allah reveals, they are the disbelievers.” [TMQ 5:44] This doctrine works because it treats people as human beings and just that, and because its sources of law are not from man. Allah (swt) says, “And among His signs is the creation of the heavens and the earth, and the variations in your languages and your colours : verily in that are signs for those who know.” [TMQ 30,22] LIE :In Islam women are not given equal rights to men. They are considered as second rate, abused, and prevented from having a say in their own affairs and public affairs.