17.7 Urithi (istikhlaf) au Utawala (‘ahd)
17.7 Succession (istikhlaf) Or Reign (‘ahd)
Khilafah haifungwi kwa kuteua mrithi au mtawala ajaye, kwa kuwa ni mkataba kati ya Waislamu na Khalifah. Bai'ah ya Waislamu na kukubali kwa yule wanayemchagua ni sharti katika mkataba wa Khilafah. Kuteua mrithi au mtawala ajaye hakulingani na kujumuisha sharti hili, kwa hiyo Khilafah haianzishwi kwa njia hiyo. Kwa hiyo, kuteuliwa kwa Khalifah atakayefuata na Khalifah aliyepo, hakumo katika mkataba wa Khilafah, kwa sababu yeye hana haki ya kuufunga mkataba huo. Pia, Khilafah ni haki ya Waislamu, si ya Khalifah, nao huufunga mkataba kwa yeyote wamtakaye. Kwa hiyo kuteua Khalifah ajaye au kumpendekeza na Khalifah aliyepo si sahihi, kwa kuwa anatoa kitu asichokimiliki. Kutoa kitu ambacho mtoaji hakimiliki ni haramu. Hivyo, Khalifah aliyepo hawezi kumteua Khalifah mwingine wa kumrithi, awe mwanawe, jamaa yake au mtu asiyehusiana naye sana, na Khilafah haifungwi kwake kabisa, kwa kuwa mkataba wake haukufanywa na wale wanaoumiliki. Hivyo ni mkataba batili wa fudhuli.
The Khilafah is not contracted by appointing a successor or heir, because it is a contract between the Muslims and the Khalifah. The pledge by the Muslims and the acceptance from the person whom they elect is a condition in the contract of the Khilafah. The appointment of a successor or heir does not suit to include this condition, so the Khilafah is not established with it. Accordingly, the appointment of the next Khalifah, by the existing Khalifah, is not included in the Khilafah contract because he does not have the right to contract it, and because the Khilafah is a right of the Muslims, not the Khalifah, and they contract it to whom they wish. So the appointment of the next Khalifah or recommending him by the existing Khalifah is not correct, because he gives something which he does not possess. Giving something which is not possessed by the giver is illegal. So the existing Khalifah cannot appoint another Khalifah to succeed him, whether he was his son or relative or a person remote to him, and the Khilafah is not contracted to him at all because its contract was not carried out by those who have it. Thus it is a redundant (fudhuli) contract.