9.1 Utamaduni wa Kiislamu
9.1 The Islamic Culture
Utamaduni wa Kiislamu ni taaluma ambazo masomo yake huchochewa na 'aqīdah ya Kiislamu (itikadi), iwe taaluma hizo zinajumuisha 'aqīdah ya Kiislamu na kuhakikisha usafi wake, kama vile elimu ya Tawhīd (ilm al-Tawheed), au zimejengwa juu ya 'aqīdah ya Kiislamu, kama vile fiqh (sheria ya Kiislamu), tafsīr na hadīth, au chochote kilichokuwa cha lazima kwa kuelewa kanuni zinazotokana na 'aqīdah ya Kiislamu, kama vile sayansi ya lugha ya Kiarabu, uainishaji wa istilahi za hadīth (mustalah al-hadīth) na sayansi ya misingi ya fiqh ('ilm al-usul).
The Islamic culture are the disciplines the study of which is occasioned by the Islamic ‘aqīdah (creed), whether these disciplines included the Islamic ‘aqīdah and what guarantees its purity such as theology (ilm al-Tawheed) or they are based on the Islamic ‘aqīdah such as fiqh (jurisprudence), tafsīr and hadīth or whatever became necessary for the comprehension of rules emanating from the Islamic ‘aqīdah such as the sciences of the Arabic language, terminological classification of hadīth (mustalah al-hadīth) and science of the foundations of jurisprudence (‘ilm al-usul).
Utamaduni wote wa Kiislamu unarejea kwenye Qur'ani na Sunnah. Ni kutoka kwake, kupitia kuzielewa kwake na kulingana nazo ndipo matawi yote ya utamaduni wa Kiislamu yamepatikana. Hizo (Qur'ani na Sunnah) pia ni sehemu ya utamaduni wa Kiislamu, kwa sababu 'aqīdah ya Kiislamu inalazimu kukubali na kushikamana na kila kilichotajwa ndani yake. Qur'ani iliteremshwa kwa Mtume ﷺ ili yeye auweke wazi kwa watu. Allah (SWT) amesema: