"Enyi watu, hakika mimi ni Mtume wa Allah ﷺ kwenu nyote." (TMQ 7:158), "Enyi watu, mcheni Mola wenu." (TMQ 4:1), "Enyi mlioamini, mwitikieni Allah (swt) na Mtume ﷺ." (TMQ 8:24), "Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga." (TMQ 2:183), "Basi atakayeshuhudia [mwezi mpya wa] mwezi huo, na afunge." (TMQ 2:185), "Na simamisheni Swala." (TMQ 2:43), "Chukua, [Ee Muhammad ﷺ], katika mali yao." (TMQ 9:103), "Zakah ni kwa ajili ya mafukara na masikini tu." (TMQ 9:60), "Na wale wanaokusanya dhahabu na fedha." (TMQ 9:33), "Allah (swt) ameruhusu biashara na ameharamisha riba." (TMQ 2:275), pamoja na maandiko mengine mengi yanayofanana. Katika haya yote, Mwenye Kutunga Sheria (swt) anawasemesha wanadamu kwa khitabu cha jumla, bila kujali kama aliyesemeshwa ni mwanamume au mwanamke. Na ujumla wa khitabu cha Mwenye Kutunga Sheria (swt) unabaki katika ujumla wake. Kwa hiyo, Shari'ah imekuja kwa ajili ya wanadamu, si kwa ajili ya wanaume kwa sifa yao ya kuwa wanaume, wala kwa ajili ya wanawake kwa sifa yao ya kuwa wanawake, bali kwa ajili ya wanadamu kwa mtazamo wa kuwa binadamu. Hivyo, kila kitu ambacho Shari'ah imeamuru kimekuja kwa ajili ya wanadamu, na chochote inachojumuisha kwa upande wa haki na wajibu ni kwa ajili ya wanadamu na ni juu yao. Hii ndiyo dalili ya sehemu ya makala inayotaja kwamba mwanamke ana haki na wajibu sawa na mwanamume, kwa sababu Shari'ah imekuja kwa ajili ya wanadamu, na mwanamume na mwanamke wote ni binadamu, wala haikuja mahsusi kwa mwanamke au mwanamume, na hivyo wawili hao ni sawa kwa upande wa khitabu cha Mwenye Kutunga Sheria (swt) kuhusu hukumu za Shari'ah kwa wanadamu.
"O mankind, indeed I am the Messenger of Allah (saw) to you all.” (TMQ 7:158), “O mankind, fear your Lord.” (TMQ 4:1), “O you who have believed, respond to Allah (swt) and to the.” (TMQ 8:24), “O you who believe! fasting is prescribed for you.” (TMQ 2:183), “So whoever sights [the new moon of] the month, let him fast it.” (TMQ 2:185), “And establish prayer.” (TMQ 2:43), “Take, [O, Muhammad], from their wealth.” (TMQ 9:103), “Zakah expenditures are only for the poor and for the needy.” (TMQ 9:60), “And those who hoard gold and silver.” (TMQ 9:33), “Allah (swt) has permitted trade and has forbidden interest(usury).” (TMQ 2: 275), amongst many other similar texts. In all of these the Legislator (swt) addresses humankind with a general address irrespective of whether the one addressed was male or female. And the generality of the address of the Legislator (swt) remains upon its generality. Accordingly, the Shari’ah came for humankind and not for men in their characteristic of being male, or for women in their characteristic of being female, rather for mankind from the angle of being human. Therefore, whatever the Shari’ah commanded came for humankind, and whatever it includes in terms of rights and obligations are for and upon humankind. This is the evidence for the part of the article which mentions that the woman has the same rights and obligations as the man, because the Shari’ah came for humankind, and both male and female are human, and it did not come specifically for woman or man, and so the two of them are equal in respect to the address of the Legislator (swt) regarding the Shari’ah rules for humankind.