Kifungu cha 139
Article 139
Serikali hairuhusiwi kuhamisha mali ya binafsi kuwa mali ya umma, kwa kuwa mali ya umma imethibitishwa na asili na sifa ya mali yenyewe, si kwa maoni ya Serikali.
The State is not permitted to transfer private property into public property, since public property is confirmed by the nature and characteristic of wealth and not by the opinion of the State.
Ushahidi ni maneno kutoka kwenye hadith iliyokubaliwa ya Mtume ﷺ kupitia Abu Bakra:
The evidence are the words from the agreed upon narration of the Messenger (pbuh) through Abu Bakra:
. إِنَّ دِمَاءكَُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ عَلَيْكُمْ حَ رَامٌ كَحُرْمَةِ يوَْمِكُمْ هَذَا فِي بلََدِكُمْ هَذَا « »... فِي شَهْرِكُمْ هَذَا .
. إِنَّ دِمَاءكَُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ عَلَيْكُمْ حَ رَامٌ كَحُرْمَةِ يوَْمِكُمْ هَذَا فِي بلََدِكُمْ هَذَا « »... فِي شَهْرِكُمْ هَذَا .
“Hakika! Damu zenu, mali zenu, na heshima zenu ni takatifu kwa kila mmoja wenu, kama utakatifu wa siku hii yenu, katika mji huu (Makka) wenu, katika mwezi huu wenu,” ambalo ni la jumla na linajumuisha kila mtu, hivyo ni haramu kuchukua mali ya mtu yeyote, awe Mwislamu au si Mwislamu, isipokuwa kwa sababu iliyowekwa na sheria. Kwa hiyo, ni haramu kwa Dola kuchukua mali ya mtu yeyote isipokuwa kwa sababu ya Shari’ah. Kwa msingi huo, ni haramu kwa Dola kuchukua mali ya mtu yeyote kuimiliki kwa kisingizio cha manufaa, au kuifanya mali ya umma kwa manufaa ya Ummah, kwa kuwa hadithi imekataza hilo, na manufaa hayafanyi kitendo hicho kiwe halali, kwa kuwa kuhalalishwa kwake kunahitaji ushahidi wa Shari’ah. Haiwezi kusemwa kwamba Imamu anaweza kufanya hivyo kama sehemu ya kusimamia maslahi ya Ummah, kwa kuwa yeye ana haki ya kusimamia mambo. Hii ni kwa sababu kusimamia mambo ni kushughulikia maslahi ya watu kulingana na kanuni za Shari’ah, wala si kushughulikia maslahi ya watu kulingana na maoni ya Khalifah. Kwa hiyo Khalifah hana mamlaka yoyote ya kuruhusu kile ambacho Allah (SWT) amekikataza, na akifanya hivyo, kitendo hicho kitachukuliwa kuwa dhuluma, ambayo atapelekwa mahakamani kwa ajili yake, na mali itarudishwa kwa mmiliki wake.
“No doubt! Your blood, your properties, and your honor are sacred to one another like the sanctity of this day of yours, in this (sacred) town (Mecca) of yours, in this month of yours”, which is general and encompasses every person, and so it is forbidden to take the wealth of any individual, whether Muslim or not, except for a legislated reason. Therefore, it is forbidden for the State to take the wealth of any individual except for a Shari’ah reason. Accordingly, it is forbidden for the State to take the wealth of any individual into its possession on the grounds of benefit, or to make it public property for the benefit of the Ummah, since the narration forbade that and benefit does not make it permitted, as its permission would require a Shari’ah evidence. It cannot be said that the Imam can do that as part of governing the interests of the Ummah since he has the right to manage the affairs. This is because the management of the affairs is the undertaking of the interests of the people according to the Shari’ah rules, and not the undertaking of the peoples’ interests according to the opinion of the Khalifah, and so the Khalifah has no power at all to permit whatever Allah (swt) forbade, and if he did so the action would be considered an injustice which he would be taken to court for, and the wealth would be returned to its owner.
Kwa msingi huu, kile kinachoitwa utaifishaji (nationalisation) hakitokani na Shari'ah kwa namna yoyote ile. Kwani ikiwa mali ina asili na sifa ya mali ya umma, basi ingekuwa wajibu juu ya Dola kuifanya kuwa sehemu ya mali ya umma, wala isingekuwa na hiari katika hilo. Kwa hiyo haitazingatiwa kuwa ni utaifishaji, bali asili na sifa ya mali ndiyo iliyoifanya kuwa sehemu ya mali ya umma kwa uhalisia. Na itakuwa haramu kwa Dola kuruhusu mali hiyo imilikiwe binafsi. Ama ikiwa mali inamilikiwa na mtu binafsi na haina sifa wala asili ya mali ya umma, basi itakuwa haramu kwa Dola kuitaifisha. Na ikiwa itafanya hivyo, itapelekwa mahakamani na mali itarudishwa kwa mmiliki wake. Hii ni kwa sababu Mtume wa Allah ﷺ alichukua tena ardhi ya chumvi kutoka kwa Abyad bin Hammal baada ya kumpa, mara tu ilipodhihirika kuwa haikuwa haina kitu cha kuchimbwa.
Based upon this, what is called nationalisation is not from the Shari’ah in any shape or form, since if a property had the nature and characteristic of public property then it would be obligatory upon the State to make it part of the public property, and it would have no choice in that, and so this would not be considered nationalisation but rather the nature and characteristic of the property meant that it was in reality part of the public property, and it would be forbidden for the State to allow it to be privately owned. As for if the property was owned by an individual and did not have the characteristic or nature of public property, then it would be forbidden for the State to nationalise it, and if it did so it would be taken to court and the property would be returned to its owner. This is since the Messenger of Allah (pbuh) took the salted land back from Abyad Bin Hammal after he had granted it to him, once it became apparent that it was not depleted.