Ibara ya 82
Article 82
Inaruhusiwa kugawanya madaraja ya mahakama kulingana na aina ya kesi. Baadhi ya majaji wanaweza hivyo kupangiwa kesi fulani za daraja fulani, na mahakama nyingine kuidhinishwa kusikiliza kesi nyingine.
It is permissible to vary the grades of courts in respect to the type of cases. Some judges may thus be assigned to certain cases of particular grades and other courts to be authorised to judge the other cases.
Dalili yake ni kwamba uamuzi (al-qadha) hukabidhiwa na Khalifah, na ni kama wakala (wakālah), wala hakuna tofauti baina yao. Uamuzi ni aina moja ya wakala, na inaruhusiwa kwa wakala kuwa wa jumla au wa kipekee. Kwa hiyo, itaruhusiwa kumteua hakimu kushughulikia kesi maalum tu, na kukatazwa kushughulikia kesi nyingine yoyote. Inaruhusiwa kumteua hakimu mwingine kuchunguza kesi za aina zote, zikiwemo zilizotajwa, hata katika eneo hilo hilo, au kuchunguza kesi nyingine zisizo zile zilizotajwa. Kwa hiyo, inaruhusiwa kuwa na ngazi mbalimbali za mahakama, na Waislamu walikuwa nazo katika zama za mwanzo. Al-Mawardi aliandika katika kitabu chake kiitwacho Al-Ahkam Al-Sultaniyyah: “Abu ‘Abd Allah Al-Zubayr alisema: ‘Viongozi hapa Basra walikuwa wakimteua hakimu katika msikiti mkuu, nao walimwita hakimu wa msikiti. Alikuwa akihukumu katika mizozo inayohusu kiasi kilicho chini ya dinari ishirini na dirham mia mbili, na alikuwa akiamuru matunzo (Nafaqah). Hakuvuka mipaka yake wala majukumu aliyokabidhiwa’.” Mtume wa Allah ﷺ alimkabidhi wengine uamuzi kwa niaba yake katika kesi moja tu, kama alipomkabidhi Amr b. Al-‘As, na alimkabidhi wengine uamuzi kwa niaba yake katika kesi zote katika mkoa fulani, kama alivyomkabidhi ‘Ali b. Abi Talib (ra) uamuzi katika Yemen. Hii inaonyesha kwamba inaruhusiwa kuwa na uamuzi maalum na uamuzi wa jumla.