Kifungu cha 96
Article 96
Usimamizi wa mambo ya serikali na ya wananchi unafanywa na ofisi, idara, na mamlaka mbalimbali, ambazo kazi yake ni kuhakikisha usimamizi wa shughuli za Dola na utekelezaji wa maslahi ya wananchi.
Management of the government’s and people’s affairs is carried out by offices, departments, and administrations, whose task is to ensure the management of the State’s business and the carrying out of the people’s interests.
Mtume wa Allah ﷺ alikuwa akisimamia mambo na kuwateua makatibu kwa ajili ya utawala wao. Hivyo, Mtume ﷺ alikuwa akiendesha mambo ya watu wa Madina, akitatua matatizo yao, akipanga mahusiano yao, akitimiza mahitaji yao, na kuwaelekeza kwenye yale yaliyowafaa. Mambo haya yote ni katika masuala ya utawala yaliyorahisisha maisha yao na kuwaondolea matatizo au mikanganyiko.
The Messenger of Allah (pbuh) used to run and carry out the affairs and appoint secretaries for their administration. Thus, the Messenger (pbuh) used to carry out the affairs of the people in Madinah, solve their problems, organise their relations, secure their needs, and direct them to that which suited them. All of these matters are of the administration issues that eased their life from problems or complications: