Ibara ya 44
Article 44
Ni sharti la kumwezesha msaidizi aliyekabidhiwa madaraka (Tafwid) kwamba uwezeshaji wake uhusishe mambo mawili: la kwanza ni wajibu wa jumla, na la pili ni uwakilishi. Kwa hiyo, ni lazima Khalifah amwambie: “Ninakuteua kwa niaba yangu kuwa naibu wangu” au maneno yoyote yenye maana kama hiyo miongoni mwa maneno yanayojumuisha wajibu wa jumla na uwakilishi. Idhini hii inamwezesha Khalifah kuwatuma wasaidizi hao kwenda sehemu maalum, au kuwahamishia sehemu nyingine na kazi nyingine kadri inavyohitajika kama msaidizi wa Khalifah, bila haja ya idhini mpya kwa kuwa yote hayo yanaingia chini ya uwezeshaji wa awali.
It is a condition for the empowering of a delegated assistant (Tafwid), that his empowerment encompasses two issues: The first being general responsibility, and the second being the representation. Accordingly, it is necessary for the Khalifah to say to him “I appoint you on my behalf as my deputy” or anything that is of a similar meaning from the wordings that encompass the general responsibility and representation. This authorisation enables the Khalifah to send the assistants to specific locations, or transfer them to other places and other work as is required as the assistant of the Khalifah, and without the need for a new authorisation since it all falls under the original empowerment.
Ushahidi wa hili ni uhalisia wa kazi ya msaidizi, kwani msaidizi wa Tafwidh, au waziri wa Tafwidh, ni yule waziri ambaye Khalifah amemteua ili kubeba jukumu la utawala na mamlaka pamoja naye. Yeye ameidhinishwa kusimamia mambo kwa mujibu wa maoni yake, na kuyaendesha kwa mujibu wa Ijtihad yake kwa kuzingatia hukumu za Shari’ah, na hivyo Khalifah humpa mamlaka ya jumla ya kushughulikia mambo na kuwakilisha. Uwakilishi hapa ni mkataba, na mikataba haisihi isipokuwa imefungwa kwa neno wazi. Kwa sababu hiyo, imewekwa kuwa sharti kwamba kumpa msaidizi mamlaka lazima kufanyike kwa maneno yanayoonyesha kuwa yeye ni mwakilishi mahali pa Khalifah na ana udhibiti wa jumla. Kwa mfano, Khalifah akisema kwake: “Nimekupa kile kilicho juu yangu, uwakilishe kwa niaba yangu”, au akisema: “Nimekufanya waziri na nimeamua uwakilishi wako”, au kwa maneno yanayofanana na hayo. Yaani, maneno hayo yanapaswa kujumuisha uwakilishi wa jumla na udhibiti wa jumla kwa namna yoyote inayoeleweka. Kwa hiyo ni lazima uteuzi wa msaidizi uwe kwa maneno yanayoonyesha uhalisia wake, ambao ni kuwa mwakilishi wa Khalifah, na kwamba anachukua kila kitu katika mamlaka ya lazima ambayo Khalifah anayo. Kwa maneno mengine, ni lazima mkataba wa uwaziri wa msaidizi ufungwe kwa maneno yanayojumuisha masharti mawili: la kwanza ni udhibiti wa jumla, la pili ni uwakilishi. Na endapo maneno hayatashughulikia waziwazi masharti hayo mawili, basi uwaziri wa msaidizi haujafungwa.