Kifungu cha 178
Article 178
Ni wajibu wa Dola kuwafundisha kila mtu mambo yale yanayohitajika kwa maisha ya kawaida, awe mwanamume au mwanamke, katika ngazi ya msingi na ya sekondari. Elimu hii lazima itolewe bure kwa kila mtu, na Dola inapaswa, kwa kadiri ya uwezo wake, kutoa fursa kwa kila mtu kuendelea na elimu ya juu bila malipo.
It is an obligation upon the State to teach every individual those matters that are necessary for the mainstream of life, male or female, in the primary and secondary levels of education. This must be provided free of charge to everyone, and the State should, to the best of its ability, provide the opportunity for everyone to continue higher education free of charge.
Ushahidi wake ni kwamba hili ni miongoni mwa maslahi muhimu na manufaa kwa watu, kwa kuwa kuwafundisha watu yale wanayohitaji katika maisha ya kawaida ni miongoni mwa maslahi muhimu, kwa kuwa huleta manufaa na kuondoa madhara. Ndiyo maana ni wajibu kwa Dola kutoa huduma kwa maslahi haya kulingana na mahitaji ya maisha ya kawaida, na kulingana na idadi ya vijana waliopo wanaohitaji kufundishwa mambo hayo. Elimu ya msingi na ya sekondari kwa watu wengi imekuwa jambo la lazima kutokana na hali ya maisha baina ya mataifa katika zama hizi, wala si tena miongoni mwa mambo yasiyo ya lazima. Kwa hiyo, ni wajibu kwa Dola kutoa elimu ya msingi na ya sekondari kwa kila mtu kwa kiwango cha yale yanayohitajika ili kushiriki katika shughuli za maisha, na ni wajibu kwake pia kulifanya hilo kuwa miongoni mwa maslahi yake muhimu. Hivyo, ni wajibu kwa Dola kuanzisha shule za msingi na za sekondari za kutosha kwa raia wake wote wanaotaka kusoma, na kuwapa bure yale wanayohitaji ili kushiriki katika mambo ya maisha. Mtume ﷺ alifanya fidia ya wafungwa makafiri iwe ni kwamba wafundishe watoto kumi wa Kiislamu, na hilo lilikuwa katika mali ya vita ambayo Khalifa anaweza kuitumia kwa maslahi ya Waislamu. Hii ni dalili kwamba kutumia mali katika elimu hufanyika bila malipo yoyote yanayopokelewa kwa kubadilishana.