Ibara ya 58
Article 58
Gavana hahamishwi kutoka mkoa mmoja hadi mwingine, kwa kuwa uteuzi wake ulikuwa kwa ajili ya usimamizi wa jumla katika eneo maalum. Kwa hiyo, ni lazima kwanza aondolewe madarakani kisha ateuliwe tena.
The governor is not moved from one province to another, since his appointment was for a general control in a specific area. Therefore, he has to be discharged first and then reappointed.
Dalili yake ni kitendo cha Mtume (rehema na amani zimshukie) kwani alikuwa akiwaondoa wakuu wa mikoa, wala haikupokewa kwamba alimhamisha mkuu wa mkoa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Zaidi ya hayo, uwaliwa ni miongoni mwa mikataba inayokamilika kwa maneno ya moja kwa moja, na mkataba wa uwaliwa unahusu mkoa au mji, ambao unaonyesha mahali ambapo wali anatawala, na mamlaka ya kutawala yanabaki kwake mradi tu Khalifa asimwondoe. Basi ikiwa hakuondolewa, anaendelea kuwa wali juu yake, na ikiwa amehamishwa kwenda sehemu nyingine, hahamishwi kutoka sehemu yake ya kwanza kwa uhamisho huo, wala hateuliwi juu ya sehemu aliyohamishiwa, kwa kuwa kutengwa kwake na sehemu ya kwanza kunahitaji neno la moja kwa moja kwamba ameondolewa katika uwaliwa juu yake, na uteuzi wake juu ya sehemu aliyohamishiwa unahitaji mkataba mpya wa uteuzi unaohusu sehemu hiyo. Kwa hiyo, inachukuliwa kwamba wali hahamishwi kutoka sehemu hadi sehemu kwa uhamisho; bali anaondolewa kutoka sehemu moja na kuteuliwa kuwa wali mpya wa sehemu mpya.
Its proof is the action of the Messenger (pbuh) since he used to remove the governors and it is not narrated that he transferred a governor from place to place. Additionally, the governorship is one of the contracts that is completed by a direct wording, and the contract of the governorship is upon the province or city, which specifies the place where the governor rules, and the powers of ruling remain with him as long as the Khalifah does not remove him. So if he is not removed, then he remains a governor over it, and if he is transferred to another place, he is not removed from his first location by this transfer and is not appointed over the location that he has been transferred to, since his separation from the first location requires a direct word that he has been removed from the governorship over it and his appointment over the place that he has been transferred to requires a new contract of appointment which is specific to that location. Accordingly, it is taken that the governor is not transferred from location to location by transfer; rather he is removed from a location and appointed to a new governorship for the new location.